MAHAKAMA YAMUHUKUMU ALIYEMUUA MAMA YAKE NA KUMTUPA KWENYE CHEMBA YA CHOO


Patric Mmasi akigongeana na wakiki wake, Peter Madeleka wakati akisubiri kusomewa uamuzi.

Mahakama kuu kanda ya Arusha imemfunga miaka 10 jela, Patric Loishie Mmasy, (26) baada kumkuta na hatia ya kumuua bila kukusudia mama yake mzazi, Ruthy Loishie Mmasi,(40).



Patric alimuua mama yake  kwa kumtoboa shingo na meno ya rato kisha kumvunja shingo ambapo aliutupa mwili wa mama yake ndani ya shimo la maji taka la nyumba yao iliyopo Njiro baada kusikia honi ya gari.

Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 15,2023 na Jaji, Angaza Mwaipopo  aliyesikiliza shauri hilo la mauaji namba 164/2022 ambaye amesema kuwa ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine .

"Je Matendo ya mshitakiwa kabla na baada ya tukio hakuonyesha anajutia yale aliyoyafanya... alijaribu kuzuia damu isitoke shingoni kwa kumfunga kitambaa lakini aliposikia kelele ya gari akamtupa kwenye shimo la maji taka," amesema jaji Mwaipopo wakati akisoma adhabu kwa Patric  na kuongeza

"Marehemu alikuwa na majeraha mawili shingoni tukio lile ni baya na ni mbaya zaidi kulifanya kwa mama yako mzazi mwanaume haitaji kumpiga mwanamke kwa namna yoyote...... nampa adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela,". 

Awali jaji Mwaipopo amesema kuwa mahakama imemtia hatiani Patric baada ya kupitia hoja za pande zote ambapo  upande wa mashitaka wenye jukumu la kuthibitisha mashitaka yanayomkabili mshitakiwa huyo walileta mashahidi 14 na utetezi wa Patric aliyejitetea mwenyewe bila kuwa na kielelezo chochote mahakama.



Maelezo ya mshiwakiwa huyo ya ukiri ndiyo yalimtia hatiani ambapo Jaji Mwaipopo  aliyanukuu kuwa "mshitakiwa alikiri polisi, alimuua mama yake baada ya mama yake kumrushia nyundo ambapo aliikwepa kisha akamfuata mama yake na rato ambapo wakati mama yake akirudi kunyumenyume alijikwaa kwenye kabati kisha akaanguka ambapo yeye akimchoma shongoni kwa nyundo,".

Jaji ameendelea kusema kuwa  kwenye maelezo hayo alikiri kuwa alichukua simu ya mama yake nyekundu aina ya tecno kisha akaitupa kwenye shimo la maji taka ambapo aliwaongoza polisi mpaka nyumbani hapo kisha vitu hivyo vikapatikana.

"Ushahidi wa shahidi wa pili ambaye ni daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu unaonyesha kuwa  kifo cha marehemu kilitokana na kukabwa shingo, kukosa hewa na alikuwa na jeraha shingoni na kupelekea shingo kuvunjika," amesema Jaji Mwaipopo waokti mahakama ikiangalia kama mshitakiwa alikuwa na nia ya kumuua marehemh na kuongeza .

"Daktari alisema jeraha lililokuwa kwenye shingo ya marehemu hawezi kusema alikufa kwa kutoka  damu nyingi  kwani mwili wa marehemu tayari ulikuwa umeshakaa muda mrefu kabla ya yeye kufanyiwa uchunguzi huo.

"Kifo cha marehemu kilitokana na kukosa hewa. Hakukuwa na uwezekano wa kusema jereha kwenye shingo ya marehemu lilisababisha kifo kwa sababu muda mrefu ulipita tokea kifo kitokee na yeye kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu .

"Maelezo ya ukiri ya mshitakiwa inaonyesha marehemu alimrushia nyundo yeye (Patric) akakwepa yeye (Patric) akamfuata marehemu akiwa na rato marehemu akawa anarudi kinyume nyume akajikwaa kwenye kabati akaanguka chini  na yeye (Patric) akamchoma marehemu  na rato shingoni. 

"Msimamo wa kisheria mauaji yanapotokea kwenye mazingira ya ugomvi nia ovu inakuwa haipo hivyo mahakama inamtia hatiani Patrick loshie Mmasi kwa mauaji bila kukusudia,". 

Baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa hilo wakili wa serikali, Eunice Makala aliiomba mahakama impe adhabu kali Patric ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojichukulia majukumu ya kuondoa uhai wa watu wengine.

 "Kutokana kwa mshitakiwa kupoteza uhai wa marehemu Taifa limepoteza nguvu kazi na marehemu alikuwa anategemewa na familia yake na watoto wawili kwa msingi huo tunaomba adhabu iwe kali," aliomba Makala 

Hata hivyo wakili wa Patric, Peter Madeleka aliiomba mahakama impe mteja wake adhabu ndogo kwani hana rekodo ya uhalifu huku akirejea kuwa alimuwa ni miongozni mwa watoto ambao walikuwa wanamtegemea marehemu.


Wakili wa mshitakiwa huyo Peter Madeleka aliiomba mahakama hiyo kumpa adhabu ndogo kabisa mteja wake huu akirejea taarifa ya upande wa jamhuri mahakamani hapo waliyoeleza kuwa Patric hana rekodi ya uhalifu.

"Mheshimiwa jaji, upande wa jamhuri pia wamesema  marehemu alikuwa na familia inayomtegemea ya watoto wawili akiwemo huyu aliyetiwa hatiani," ameeleza  Madeleka akiomba adhabu hiyo iwe ndogo na iuongeza

"Na kosa limethibitika kutendeka katika mazingira ambayo hapakuwa na nia ovu na kwa kuwa ni hiari ya mahakama kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria mheshimuwa jaji kwa unyenyekevu mahakama yako itumie mamlaka yake kutoa adhabu ndogo sana kwa sababu kwa kosa hili  adhabu ya juu ni kifungo cha maisha jela. Ni ombi letu apewe kifungo kidogo   kabisa hata cha  miezi sita jela ili mtiwa hatiani aweze kujifunza na kujutia kosa alilofanya,

Awali akisoma mwenendo wa shauri hilo Jai Mwaipopo alisoma utetezi wa Patric alioutoa manakamani hapo mara baada ya mahakama kumuona ana kesi ya kujibu ambaye mbali ya kukana kuishi kwenye nyumba hiyo na mama yake lakini pia alisema hakuna shahidi aliyeieleza mahakama kuwa alimumuoa akimuua 


Mahakama iliona mshitakiwa ana kesi ya kujibu ambaye alijitetea mwenyewe bila kutoa kielelezo aambaye katika utetezi wake alisema kuwa Desemba 24,2021 alijikuta akiwa kituo cha polisi na aliteswa na polisi wakiongozwa na shahidi watatu Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha, Gwakisa wakimlazimisha akubali kumuua marehemu.

Patric aliieleza mahakama kuwa akiwa hapo ndipo Dewemba 27,2021 alisikia kwa mara ya kwanza kuwa mama yake amekufa lakini licha ya mateso alikataa kukiri kuhusika ambapo desemba 28,2021 waliacha kumtesa baada ya kumuona amechoka na Januari 17,2022  alifikishwa  mahakamani.

 
Mshitakiwa anasema hakuwaongoza polisi kwenda hyumbani kwa mama yake wala hakuwepo wakati mwili wa marehemu unapatikana wala siku  nyundo, rato na simu ya tecno nyekundu kama ushahidi ulivyotolewa na hawatambui wala kuwafahamu shahidi wa tano na saba licha ya wao kudai kuwa ni ndugu wa mama yake na hajawahi kukiri kuua na anasema hakukuwa na mtu aliyesema kuwa aliyesema alimuona akimuua marehemu.

Jaji alisema kuwa mwili wa marehemu ulionyesha kuwa umechomwa shingoni upande wa kulia na kitu kwenye ncha kali. Ukweli ni kuwa amekufa kifo kisicho cha kawaida kutokana na majeraha aliyokuwa nayo. Swali je  mshitakiwa ndiye alisababisha kifo cha marehemu na alikuwa na nia ovu.

"Mshitakiwa anashitakiwa kwa mauaji na upande wa mashitaka unawajibu wa  kuthibitisha kosa hilo bila kuacha mashaka yoyote,"anasema Jaji Mwaipopo na kuongeza. 

"Ushahidi uliopo mbele ya mahakama ni ushahidi wa mazingira, mahakama inaweza kumtia hatiani mshitakiwa endapo ushahidi huo utaungana.Ushahidi unatakiwa ufikie hitimisho moja kuwa mshitakiwa ana hatia bila kuacha mashaka yoyote.

"Ushahidi wa mashitaka unaegemea kuwa mshitakiwa alikuwa akiishi nyumba moja na marehemu na atakuwa ndiye mtu wa mwisho kuonana naye na maelezo yake ya ukiri yaliyowezesha kupatikana kwa rato, nyundo na simu.


Patric ambaye muda wote akiwa mahakamani hapo alionekana kuwa mtulivu huku akifuatilia hukumu hiyo iliyotolewa kuanzia majira ya saa 11 jioni mpaka saa moja usiku  ambapo ndugu wa marehemu, Ruthy akiwepo mtoto mwingine Monica walikuwa wamejaa kwenye chumba hicho cha mahakama kuanzia majira ya saa nane mchana ambapo ndiyo muda wa awali ambao mahakama ilipanga kutoa uamuzi huo.

Mara baada ya uamuzi huo askari magereza walimchukua Patric na kuondoka naye huku ndugu wa marehemu wakitoka nje kimya wakiwa hawako tayari kutoa maoni yoyote juu ya uamuzi huo.

Tayari wakili wa Patric, Madeleka amesema kuwa hawajaridhika na uamuzi huo hivyo ataka rufaa.

0 Comments:

Post a Comment