Na Gift Mongi, Moshi
Huenda ni muendelezo wa wa kutangaza vivutio vya utalii tulivyo navyo kazi ambayo imeasisiwana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye utawala wake.
Itakumbukwa Rais Samia alipoingia madarakani alikuja na nia njema ya kuhamasisha utalii ili kuongeza pato la taifa.
Kwa jitihada hizi ndipo wazo la uanzishwaji wa filamu ya 'THE ROYAL TOUR' ikiwa na maana kututangaza huko ulimwenguni ambapo alilfanikisha
Katika minajili hiyo mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima naye ameunga mkono jitihada hizo kwa aina yake ambapo anasisitiza Watanzania kulitumia shirika la ndege ili kuleta kulikuza na kulitangaza taifa.
Akiwa safarini kwenda nchini China ambapo pia ametumia ndege ya shirika la ndege nchini (AIR TANZANIA)anasema nchi imefungua fursa lukuki na hivyo wananchi wanaweza kuzichangamkia.
Aidha katika hatua nyingine Shirima ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha YURESHI
amewataka watanzania kumuunga mkono rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha utalii nchini kwa kutumia shirika la ndege nchini.
'Tuunge mkono jitihada zinazofanywa na serikali kuhamasisha utalii lakini tuhamasishe pia kutumia kwa Shirika letu la ndege katika kukuza utalii'amesema
Ameeleza maendeleo mbalimbali yanayo fanyika nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya vya mama na mtoto, madawa na vifaa tiba kuwa ni jitihada za serikali kuakikisha wananchi wanasogezewa huduma karibu yao.
Kadhalika mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini amesema , Rais Samia amewekeza kwa kwenye elimu nchini hali ambayo inawafanya watanzania kusoma bure kuanzia elimu ya msingi hadi secondari huku akitoa mikopo katika vyuo vikuu na kati.
Kuna kipindi tulikuwa hatuna ndege inayoruka lakini sasa dunia inaanza kutuelewa vizuri hakika hapa kama taifa tumepiga hatua na serikali Ina haki ya kusifiwa katika hili'Amesema Charles Mshiu mdau wa usafirishaji mjini Moshi
0 Comments:
Post a Comment