WANACHAMA na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA) wakisubiri kuanza kusomwa kwa hukumu kesi ya Halima Mdee na wabunge wenzake 18 waliofukuzwa uanachama wa chama hicho.
Uamuzi huo unasomwa leo Desemba 14,2023 na Jaji, Cyprian Mkeha,kwenye mahakama Kuu kanda ya Dar Es Salaam.
Mawakili wa upande wa Chadema Dickson Matata, Tito Magoti, Deogratius mahinyila na Seleman Matauka.
Upande wa Jamhuri unawakilishwa na mawakili wa serikali, Jesca Shangala, Hangi Chana na Rose Chilongoz
Waleta Maombi wanawakilishwa na mawakili Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge na Edson kilatu.
Kwa niaba ya wajibu maombi naitwa i na Jesca shengema na leonia maneno na Tause Kilonzo
Upande wa mjibu maombi wa kwanza ni :-
Dickson matata, Selemani Matauka, Tito magoti, Deogratius Mahinyila
Kwa upande wa waleta maombi ni Aliko mwamanenge , Edson Kilatu, Joy Mwakapila, Humphrey Malenga, na Gilbert Masaga!
Mleta maombi namba tisa Conjesta Rwamlaza ndiye pekee aliyefika mahakamani ambapo kwenye shauri hilo kuna waleta maombi 19.
Jaji: niwapeni Pole tumepata Ukumbi Mdogo Lakini tutaendelea hivyo hivyo kuutumia hivyo, na nitasoma Uamuzi ila uamuzi ni mrefu kidogo naombeni mvumilie! Na nitausoma kwa lugha niliyoundika na baadae nitaufafanua kwa lugha nyingine.
Msipate tabu kuhangaika uamuzi baada ya kuusoma utakuwa TANZII hivyo unaweza kuusoma kwa utulivu!
Waleta Maombi walikuwa wanachama wa Chadema
Jaji anaanza kusoma uamuzi wake kwa kurejea masuala yaliyojiri kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Jaji anarejea Sheria mbalimbali na Katiba ya nchi ambazo zinakipatia Chama cha siasa kupata idadi ya Wabunge wa Viti Maalum kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Katiba.
Jaji anaeleza kwamba tarehe 24.11.2020 waleta maombi walionekana wakiapa kuwa Wabunge wa JMT na tarehe 27.11.2020 Katibu Mkuu aliutangazia umma kutokutambua Wabunge hao.
Jaji anasema kuwa siku hiyo tarehe 27.11.2020 Katibu Mkuu aliwaandikia kuwaita.
Jaji: Anaorodhesha vifungu mbalimbali ambavyo vimezingatiwa na waleta maombi katika kuwasilisha maombi yao.
Jaji: Anaendelea kwamba maombi hayo yalipingwa na Bodi ya Wadhamini ya Chadema na kutaja orodha ya Mawakili waliowasilisha Pande zote.
Jaji: Anaendelea kusoma hatua mbalimbali zilizofuatwa katika mwenendo wa shauri hili kwa kuwaita waleta maombi mbalimbali pamoja na mapingamizi yaliyowasilishwa.
Jaji anasoma hoja za Mawakili wa Pande zote na mwenendo wa shauri hili kwa kuzingatia yote yaliyofanyika kabla na baada ya kina Halima kufukuzwa na Kamati Kuu ya Chadema, walivyokata Rufaa kwenye Baraza Kuu la Chama na hatua zilizochukuliwa.
Jaji anaeleza Hoja zote zilizowasilishwa na Waleta maombi
Jaji: Yafuatayo nimeyabaini
1. Je majibu maombi alikuwa na haki ya kushughulikia suala husika kwa dharura na kuwapa waleta maombi hakibya kusikilizwa!?
2. Je waleta maombi walipata Haki ya kusikilizwa!?
3. Je Baraza Kuu la Chama lilitimiza wajibu wake Kwa Haki kwa mujibu wa Katiba!?.
Jaji: Majibu Maombi alikuwa na haki ya kuchukua hatua kwa mujibu wa Ibara 6.5.1 (d) ya Katiba ya Chama.
Waleta maombi walikiri kwamba walipokea Wito wa Kufika Mbele ya Kamati Kuu, hakuna Mleta maombi hata mmoja aliyetoa taarifa za tishio la amani kwa vyombo Vya Usalama.
Hakuna ushahudi wowote kuwa Waleta Maombi walikuwa Dodoma tarehe 27.11.2020
Ni wazi kwamba Majibu maombi alitekeleza ombi la Waleta Maombi kwa kugamisha Ukumbi wa Kikao kwenda Bahati Beach Ledger Plaza.
Kuhusu Hati ya Mashitaka
Jaji anasema Hati ya Wito uliotolewa na mjibu maombi ilikuwa na hoja zote za kujibiwa na waleta maombi.
Jaji anaanza kusoma uamuzi wake kwa kurejea masuala yaliyojiri kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Jaji anarejea Sheria mbalimbali na Katiba ya nchi ambazo zinakipatia Chama cha siasa kupata idadi ya Wabunge wa Viti Maalum kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Katiba.
Jaji anaeleza kwamba tarehe 24.11.2020 waleta maombi walionekana wakiapa kuwa Wabunge wa JMT na tarehe 27.11.2020 Katibu Mkuu aliutangazia umma kutokutambua Wabunge hao.
Jaji anasema kuwa siku hiyo tarehe 27.11.2020 Katibu Mkuu aliwaandikia kuwaita.
Jaji: Anaorodhesha vifungu mbalimbali ambavyo vimezingatiwa na waleta maombi katika kuwasilisha maombi yao.
Jaji: Anaendelea kwamba maombi hayo yalipingwa na Bodi ya Wadhamini ya Chadema na kutaja orodha ya Mawakili waliowasilisha Pande zote.
Jaji: Anaendelea kusoma hatua mbalimbali zilizofuatwa katika mwenendo wa shauri hili kwa kuwaita waleta maombi mbalimbali pamoja na mapingamizi yaliyowasilishwa.
Jaji: Kwa kuzingatia mashauri mbalimbali niliyoyapitia,
Jaji anasoma Katiba ya Chadema Ibara ya 5 .4.3 na Ibara ya 5.4.4 na Kanuni ya 6.5.1(a) na (d) na 6.5.3
Na kutoa Tafsiri kwa kingereza.
(Ikumbukwe Kamati Kuu iliwafukuza kwa Kanuni 6.5.1(d))
Jaji: Kwa kuzingatia mazingira yaliyowekwa na Katiba ya Chadema Ibara 5.4.3 na 5.4.4 Kamati Kuu imepewa Mamlaka ya kufukuza mwanachama na kwa Kanuni ya 6.5.1(d)
Kwa hiyo Katibu Mkuu aliwaandikia barua ya Wito Waleta Maombi tarehe 25.11.2020 (ANAISOMA)
Jaji: Barua hiyo ya Wito ilipokelewa na Waleta maombi wote, ambao waliwasilisha maombi ya kuahirisha kikao.
Jaji: Wakiwa Wanachama wa Chadema, na bila kuzingatia kupokelewa maombi yao ya kuahirisha kikao, HAWAKUTOKEA KWENYE KIKAO CHA KAMATI KUU.
Jaji: Kuhusu hoja ya Usalama wao, ukweli ni kwamba Mjibu maombi (Chadema) alifuatilia na kuhamisha Ukumbi wa Kikao na kuwa Bahari Beach's Ledger Plaza.
Jaji: Kuhusu kuwa kwao Dodoma hakukuwa na ushahudi wowote juu ya Waleta Maombi kuwa Dodoma.
Jaji: Kwamba Waleta Maombi hawakujulishwa kuhusu kuhamishwa Ukumbi, naona sio kweli kwa kuwa barua za kuwajulisha mabadiliko hayo ni ya tarehe 26.11.2023, ikionyesha mjibu maombi alitekeleza ombi lao.
Jaji: Kuhusu kauli ya Mwenyekiti Freman Mbowena Kat ibu Mkuu, John Mnyika Nina maoni yafuatayo kwamba hakuna ushahidi wowote kwamba kauli zao zingewafanya wawe na upendeleo wowote wakiwa wanatekeleza majukumu yao kwenye vikao.
Jaji: Ni wazi kwamba kwa kutikuthibitisha kuwa kwao Dodoma, Waleta Maombi waliamua kwa kuipoteza Haki Yao wenyewe ya kusikilizwa
Jaji: Na kwa hiyo sio kweli kwamba hawakupewa Haki ya kusikilizwa, Bali waliamua wenyewe kuipoteza haki hiyo.
Jaji: Kwamba Hali ya Udharura iliisha walipoapa kuwa Wabunge, sio sahihi kwa sababu mwenye Mamlaka ya kuamua suala la dharura au sio dharura ni Kamati Kuu ya Chadema kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.1(d)
Jaji: anarejea kesi mbalimbali kutoka UK, India nk.
Jaji: Na kwa hiyo naona kwamba Mjibu maombi (Chadema) alikuwa sahihi katika kushughulikia suala linalolalamikiwa na Waleta Maombi.
Na kwamba Waleta Maombi waliamua wenyewe kutokuitumia Haki Yao ya kusikilizwa.
Jaji: Kwamba Waleta Maombi hawakusikilizwa kwenye Baraza Kuu la Chama, naona sio kweli kwa kuwa ni wazi kuwa fursa zote za kusikilizwa zilikuwa wazi kwao na hawakuzitumia.
Jaji: Kwamba Waleta Maombi walikuwa Wabunge na kwa hiyo suala lao lilipaswa kushughulikiwa kwa kuzingatia miongozo ya Kibunge, Kamati ya Maadili ya Chadema haijapewa Mamlaka ya kushughulikia masuala ya kinidhamu ya Wabunge.
Jaji: Rejea zote za kisheria walizozifanya Waleta Maombi haziwasaidii kwa kuwa ni Rejea ambazo haziwahusu Wabunge wa Viti Maalum.

Jaji: Kuhusu hoja ya THE LAW OF IMPARTIALITY, anarejea kesi kadhaa, pamoja na hoja za Wakili wa Mjibu Maombi.
Jaji: Anarejea kesi kadhaa tena, naona kwamba kwa Wajumbe wa Kamati Kuu kuwa wajumbe wa Baraza Kuu ni wazi kuwa wasingeweza kutenda bila Upendeleo.
Jaji: Na kwa maana hiyo sikubaliani na hoja za Wakili wa Mjibu Maombi wa kwanza, kwa kuwa hakuna mahali POPOTE kwenye Katiba ya Chadema kwamba Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wataamua Jambo Kisha wakashiriki kikao cha Rufaa kwenye Baraza Kuu.
Jaji: Kwa hiyo naona Kwamba, Baraza Kuu lilikwenda kinyume na Kanuni ya Kawaida ya kutokupendelea (The Law of Impartiality).
Jaji: Ninaona kwamba kesi hii inaangukia katika MANDAMUS
Jaji: Baraza Kuu lilipaswa kufanya kazi ya kimahakama na badala yake walifanya maamuzi kwa kuzingatia ujumla wake na Katiba yao.
Jaji: Naona kwamba maombi ya Waleta Maombi yamezinfatia hoja za Msingi za UFANISI wa chombo cha Maamuzi.
Jaji: Natoka Amri zifuatizo MAAMUZI YA BARAZA KUU YAMEFUTWA.
Jaji:Hili ni shauri kuwa nafuu mbili zinaweza kutolewa
1. Sijafuta Uamuzi wa Kamati kuu
2. Nimefuta uamuzi wa Baraza kuu! ( Certiorari)
Lakini pia nimetoa Amri ya kuamuru CHADEMA kizingatie Kanuni Asilia za haki! ( Mandamus)
Mwisho ni kuwa kila upande ubebe gharama zake na
Uhakika wa Rufaa upo wazi!
0 Comments:
Post a Comment