Leo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili. Ibada hiyo iliyoongozwa na Padre Dionis Paskal Safari ilikuwa na ujumbe wa amani na umoja.
Baada ya ibada, Dkt. Mpango ametoa wito kwa Watanzania kutumia mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji. Amesema matumizi mabaya ya mitandao hiyo yamesababisha madhara kwa watu wengi, hivyo ni muhimu kila mmoja kutumia mitandao hiyo kwa kuzingatia maadili na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.
Makamu wa Rais amewashukuru waumini kwa sala zao na kuwahimiza waendelee kumuombea ili awezoe kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Hii ni mara ya kwanza Makamu kuonekana hadharani kwani kwa zaidi ya mwezi mmoja amekua haonekani hali iiyoibua minong'ono miongoni mwa wananchi waliotaka kujua alipo kiongozi huyo wa juu baada ya Rais .
Minong'ono hiyo ilimlazimisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa taarifa kuwa Makamu wa Rais yuko salama na anaendelea na majukumu yake kikamilifu.
Hii ni hatua muhimu inayojenga imani kwa umma kuhusu afya na utendaji wa Makamu wa Rais, na inaonesha umuhimu wa mawasiliano ya wazi na uwazi katika uongozi wa nchi.

.jpg)


0 Comments:
Post a Comment