DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 KUZINDULIWA KESHO

 

Na Mwandishi wetu- Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kuzindua maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inalenga kuweka muktadha wa maendeleo ya Kitaifa katika mwelekeo wa makubaliano  na mipango ya Kikanda na Kimataifa.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  Ummy Nderiananga (kushoto) akizungumza kuhusu Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika na Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo mwaka  2050  wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule ofsini kwake Jijini Dodoma (kulia).


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na  Uratibu, Ummy Nderiananga  amesema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Dodoma  kuelezea kuhusu  maandalizi ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika na Mkutano wa Kwanza wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akieleza jambo  kuhusu Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika na Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo mwaka 2050 yatakayofanyika Jijini Dodoma.




“Shughuli za maandalizi ya maadhimisho haya zinaendelea vizuri na ya  mwaka huu hatutafanya tu maadhimisho kama ilivyozoeleka lakini itakuwa tofauti ambapo tutaungana na wenzetu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji kufungamanisha na Dira ya Maendeleo ya Taifa tutaanza 2025 hadi 20250. Miaka 62 ya Uhuru wetu imebebwa na kauli mbiu ya Umoja na Mshikamano ni chachu ya Maendeleo ya Taifa letu,” Amesema  Ummy


Waziri, Ummy ameongeza kwamba kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya  smwaka  2025  yapo  mafanikio mengi ambayo yamepatikana yakiwemo sekta ya elimu kuimariska, Afya pamoja na uwezeshaji wananwake katika maeneo mbalimbali.


“Liko eneo la kuwawezesha wanawake leo tunaye Rais  mwanamke  jasiri na mahiri Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan  hivyo tunaendelea  kumpongeza kwa miongozo na maelekezo yake  ambayo yameleta mfungamano huu pamoja na utayari na utashi wake  wa kisiasa,”Ameeleza. 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho na Shrerehe za Kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu  Batholomeo Jungu (aliyesimama) akifafanua jambo kuelekea  maadhimisho ya Sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika na Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo mwaka 2050 ( Kushoto) ni Mkurugenzi wa Bunge na Siasa katika ofisi hiyo, Raymond Kaseko.


Kadhalika alisema uzinduzi huo utafanyika kwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.



“Siku hiyo  hiyo kutakuwa na maonesho nje ya ukumbi ambayo yatashirikisha vikundi vya wajasiriamali ,taasisi na idara za Serikali pamoja na Wizara  kwahiyo nitumie fursa hii kuwakaribisha wananchi wa Mikoa jirani wanakaribishwa kushiriki tukio hilo la aina yake na lenye historia kubwa katika dira ya maendeleo ya Nchi.


Katika hatua nyingine Mhe, Ummy amebainisha kwamba Mkutano huo wa kwanza wa Kitaifa wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utaambatana na upokeaji wa taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, uzinduzi wa ukusanyaji maoni ya wadau ya dira 2050 ambapo maoni ya wadau yatakusanywa kwa njia ya simu za mkononi, mahojiano na dodoso la mtandaoni.



“Shughuli zingine zitakazofanyika ni utambulisho wa timu Kuu ya Kitaifa ya dira na utambulisho wa Wajumbe wa Tume ya Mipango kwasababu a dira hii inajenga mshikamano na umoja wa kitaifa pamoja na makubaliano kuhusu vipaumbele vya nchi,inawezesha muunganiko wa sera, mipango na mikakati mbalimbali ya kisekta na Mamlaka za Serikali za Mitaa,”Amefafanua

0 Comments:

Post a Comment