MWANAHARAKATI AWABURUZA MAHAKMANI AG, DPP

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la CILAO, Odero Charles Odero

MAOMBI ya Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la CILAO, Odero Charles Odero ya kukata rufaa nje ya muda kwenye kesi ya kutaka mtuhumiwa akamatwe baada ya upelelezi kukamilika imepangwa kusikilizwa Novemba 2,2023 kwenye mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam. 



Maombi hayo yamepangwa kusikilizwa majira ya saa 3 asubuhi mbele ya Jaji, Abdi Kagomba ambapo wajibu maombi ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (AG) na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini, (DPP.) 

Odero anaiomba mahakama kufungua maombi hayo ya rufaa nje ya muda ili aweze kufungua shauri la rufaa baada ya kutoridhika uamuzi wa mahakama kuu kanda ya Tanga ambayo ilitupilia mbali maombi yake ya kutaka mtuhumiwa akamatwe baada ya upelelezi kukamilika.

Uamuzi huo ulitolewa Desemba 19,2022 kwenye Kesi namba 20/2021 ambapo mahakama  Ilisema kuwa mlalamika ambaye ni Odero  hakuonyesha ushahidi au kiapo chake kuhusu hayo matendo aliyokuwa akiyalalamikia.

Kwenye shauri hilo walikuwa wakilalamikia matendo ya DPP ya kuwakamata na kiwafungulia  watu mashitaka bila kukamilika kwa upelelezi au uchunguzi.

Anadai matendo hayo yanakiuka haki za binadamu kwani kama umemkamata kwa tuhuma fulani ambapo mkifika mahakamani kila kesi inapofika mahakamani upande wa DPP wanasema upelelezi haujakamilika.

Anadai kuwa mtuhumiwa analazimika kurudishwa mahabusu kwa wiki mbili ndipo arudi mahakamani na inaweza kuendelea hivyo hata miezi miwili au sita au miaka minne.

Odero amewaeleza waandishi wa habari jijini Arusha kuwa aliamua kulirejesha shauri hilo mahakamani baada ya kujadiliana na wakili wake,  John Seka ambaye septemba 26,2023 alianza taratibu za kukata rufaa hiyo mahakamani.

"Kama NGO inayotetea haki za binadamu tukaona ni vema twende mahakamani kuiomba mahakama iweze kuingilia kati suala hili na ione kwamba mtu akamatwe tu pindi upelelezi wa kesi yake unapokamilika," amesema Odero na kuongeza.

"Mahakama iko pale kwa ajili ya kusikiliza kesi na kutoa haki lakini matendo hayo si CILAO peke yetu tuliona hilo ..... hata hayati John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania wa awamu ya tano aliliona hilo na kuna wakati alilizungumzia,".



0 Comments:

Post a Comment