Chuo cha Ufundi Arusha na Benki ya Dunia Kuwawezesha Vijana Kujikwamua Kiuchumi


Chuo cha Ufundi Arusha kwa ushirikiano na Benki ya Dunia vimezindua mikakati ya kuwawezesha vijana kujiondoa katika umaskini na kujenga uchumi imara katika nchi za Afrika. 

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, Oktoba 10,2023, Mussa Chacha, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, alisema kuwa kuwaelimisha vijana kuhusu jinsi ya kutumia maarifa waliyoyapata vyuoni kutawasaidia kuanzisha ajira zao na kuwa na mafanikio kiuchumi.


Nathan Belete, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Malawi, Zambia, na Zimbabwe, alibainisha kuwa wamekutanisha vijana kutoka nchi hizo nne kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya ujuzi walioupata vyuoni katika kushughulikia changamoto za kijamii. 

Benki ya Dunia imejitolea Dola bilioni 1.5 kuisaidia sekta ya elimu Tanzania, ikiwa ni sehemu ya jitihada zao za kuboresha elimu na kuwapa vijana fursa za kujifunza.


Ananilea Lema na Donald Mwakatoga, wahitimu wa Chuo cha Ufundi Arusha, wamesimulia jinsi mafunzo waliyoyapata yalivyowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuwa na mafanikio katika maisha yao ya kujiajiri.


Tutakuwa tukiendelea kufuatilia kwa karibu jinsi juhudi hizi zinavyoleta mabadiliko chanya kwa vijana na uchumi wa nchi za Afrika

0 Comments:

Post a Comment