UN WOMEN YAWANOA WANAWAKE ARUSHA

SHIRIKA la Umoja wa mataifa la Wanawake  linalojihusisha na kuwajengea uwezo wa Uongozi na haki za Kiuchumi,UN Women Leader ship and Economy light, limeanza kuwanoa Wanawake waweze kujiamini na kushiriki kwenye nafasi mbalimbali za Uongozi kuanzia ngazi za Vitongoji hadi Wilaya.



Mratibu wa Shirika hilo Mkoa wa Arusha,Blandina Nkini,ameyasema hayo Jana ,alipokuwa akizindua rasmi utekelezaji wa mpango huo kwenye Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa,ulioshirikisha madiwani Viti maalumu,Wenyeviti wa majukwaa ya Wanawake,Wenyeviti wa mabaraza ya Ardhi kata na wenye ulemavu.


Nkini,ambae pia ni afisa maendeleo ya Jamii Mkoa Mkoa wa Arusha ,amesema mradi huo unatekelezwa Katika mikoa ya Arusha,Singida,Dar es Salaam, Lindi na Mtwara,Katika mkoa wa Arusha ,mradi huo unatekelezwa Katika Wilaya za Arusha, Karatu na Monduli,ambapo Kila halmashauri inatoa kata mbili .


Amesema kuwa mradi huo umeaanza mwaka 2022 na utafikia mwisho mwaka 2026 unalenga kuwajengea Wanawake uwezo wa kuwa Viongozi na kujiimarisha  kiuchumi na kupitia mradi huo Wanawake wanaweza kuingia kwenye kinyanganyiro katika nafasi yeyote ila ya Uongozi na kuinuka kiuchumi .


Amesema kuwa mafunzo hayo yanaratibiwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi za wilaya lengo la mafuunzo hayo ni  kufahamiana na kupeana mbinu za kutekeleza sanjari na kuelimisha Wanawake kuanzia ngazi za Vitongoji hadi kata ili wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi ili ifikapo mwaka 2024 na 2025 waweze kugombea.


Amesema kuwa mwaka 2024  ni mwaka wa uchaguzi wa Viongozi wa Serikali mitaa na mwaka 2025 ni uchaguzi mkuu hivyo mafuunzo hayo  yatawezesha kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na hivyo kuondoa  mfumo dume unaowanyima fursa ya kugombea Kwa kutambua kuwa sauti zao ni muhimu  kusikia kwenye maamuzi mbalimbali ya Serikali na Jamii.


Mchango wa Wanawake kwenye Uongozi ngazi za Vitongoji hadi kata ni mdogo sana na huko ndiko kunakofanyika maamuzi hivyo mradi huo ni suluhisho kwa kuwa unawajengea uwezo ili wawe Viongozi.


Amesema kuwa chimbuko kubwa la mtizamo hasi  ni Wanawake wenyewe na ili kuiondoa ni jukumu lao  na kupitia mafuunzo hayo  yatawezesha kupambana na mfumo kandamizi  na potofu unaowakosesha fursa za kuwa Viongozi. .



Washiriki wameomba Maafisa Ardhi kutembelea Vijijini ili kutoa elimu Kwa mabaraza ya Ardhi ya kata ili kutatua changamoto za urithi wa Ardhi kwa jamii pia elimu itolewe kwa Viongozi wa Mila ambao bado ni wagumu kubadilika .


Ardhi ni swala mtambuka  hivyo watafute  mbinu mbalimbali zitakazowawezesha kuwabadilisha  Wanaume waweze kukubali kutoa mirathi ya Ardhi kwa wenza wao na hivyo kuondoa migogoro inayojitokeza  kwenye familia zetu na hivyo kuondoa changamoto zilizopo.

0 Comments:

Post a Comment