MKUU WA USALAMA BARABARANI AKOSHWA NA ATC, ATAKA VYUO VINGINE KUIGA

 

CHUO Cha Ufundi Arusha, (ATC) kimepongezwa kwa juhudi zake katika kuzalisha walimu wa udereva wenye sifa na vigezo vinavyokubalika kupitia ili kukabliana na changamoto ya ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva ambazo ni asilimia 80 ya ajali zote zinazotokea hapa nchini.

Aidha, Jeshi la polisi nchini limezifungia shule 124 za udereva zilikosa sifa idadi ambayo ni sawa na asilimia 60 ya shule zote 130  ambapo kwa sasa shule 106 ndiyo zimekidhi vigezo na zina sifa na  zinaendelea kutoa kutoa mafunzo.


Hayo yameelezwa leo, Septemba 15,2023 Kamanda wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi, Ramadhani Ng'anzi wakati alipotembelea chuo hicho kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kuzungumza na mawakala wa chuo hicho.

"Tulisema ule mtindo wa kugeuza kioski unaandika 'AZ driving school' hapa kuna bar hapa kuna saloon hapa kuna duka halafu 'driving school' ipo katikati tumekataa huu si mfumo wa shule ya udereva tunataka dereva atakayewekewa mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishwa," amesisitiza Ng'anzi na kufafanua 

...Au unakuta gari ya kujifunzia haijakaguliwa ni mbovu, shule haina vifaa. Zote tumezifungia na tukawapa miezi mitatu watengeneze miundombinu ya kufundishia wakishindwa hivyo tutawapokonya leseni,".


"Baada ya kifanya ukaguzi tukawataka warekebishe mapungufu waliyokuwa nayo ambapo tutakagua tena baada ya miezi miwili tukiona vinakidhi tutawaruhusu waendelee na wale ambao hawatakidhi tena vigezo tutawapokonya kabisa leseni zao waanze utaratibu upya wa kuziomba kwa kuleta maombi,".

"Na muda huo ulikamilika mwezi Agosti ndiyo sababu mnaona tumeanza kukagua ATC na mawakala wao wpte nchi nzima,".

Sababu kuu za ajali ni uzembe wa madereva asilimia 80 ya ajali zinazotoka chanzo ni uzembe wa madereva huwa wanatengenezwa kwa kuandaliwa katika vyuo vinavyotambulika.

Amesema chuo cha Ufundi Arusha kimepewa hadhi ya kuandaa madereva wa ngazi mbalimbali kuanzia leseni ndogo mpaka leseni ya juu ambapo hivi karibu polisi walihakiki madereva wa daraja C wale wanaendesha mabasi ya umma na daraja E wanaoendesha magari ya mizigo.

"Baada ya kuona madereva wengi hawana sifa tukaona ni vema vyuo vya udereva vikajiimarisha zaidi ili viweze kuwapokea madereva na kuwafundisha ili mwisho wa siku huko barabarani tuwe na madereva mahiri na wasiwe chanzo cha ajali barabarani,"amesisitiza Ng'anzi na kuongeza.

...ATC wameamua kushiriki  zoezi la mapambano ya kuondokana na ajali za uzembe wa madereva kwa kushirikiana na mawakala wao kwa kuzalisha walimu wa kutosha wenye sifa na vigezo vinavyokubalika.Sisi tunataka kuona viwango vya ufundishaji vinasambaa kutoka hapa kwenye shina (ATC) mpaka kwa mawakala wao kote nchini,".

"Leo tumefika kukagua madarasa, mitambo na wakufunzi wao,  mwisho wa siku tutaongea na mawakala wao kuwa viwango tulivyovikuta hapa hivyohivyo tukavikute tutakapoenda kukagua vyuo vyao,".

"Tunaamini vitu vyote tulivyoona hapa ATC vifaa vya kufundishia michoro na alama za barabarani tutaenda kuvikuta kwa mawakala walio chini ya ATC. Wakala ambaye hatakidhi vigezo na masharti vilivyowekwa hatutasita kumfutia leseni,".

Ng'anzi anaeleza aina ya madarasa yanayokidhi vigezo kuwa ,"yanatakiwa yawe na ukubwa wa futi 20 kwa 20, liwe na ubao, picha za alama za barabarani na vifaa vya kufundishia kama 'stimulator' na mashine na magari ya kufundishia. Hapa tumeona mabasi ya aina mbalimbali malori na wakufunzi ambao wamehitimu mafunzo ya kufundisha madereva,".

Akatolea mfano wa baadhi ya shule za udereva zisivyozingatia kanuni za ufundishaji " Unakuta kigari kimoja kimejaza madereva 15 wanapewa kuendesha mita mbili anashuka huyu huwezi kusema ni dereva tutakayemuamini tunataka dereva yule ambaye kweli amehitimu anajua kujihami, anajua sheria na alama za barabarani na kuwalinda watumiaji wengine wa barabara,".

"Wajue matumizi ya gari yenyewe unakuta dereva hajui kwa nini gari inawekwa oil au maji na matairi yawe namna gani.
Akijua haya inamfanya zaidi ya kujua kuendesha gari lakini anakuwa na maarifa mengine juu ya gari,".



 Kwa upande wao mawakala hao wa ATC akiwemo, Mkurugenzi wa Future world driving school ya jijini Dar es Salaam, Mkola amesema wao kama mawakala wanafahamu changamoto ziizopo kwenye fani hiyo lakini ikiwemo ukosefu wa shule zanudereva kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini.

"Mnafahamu wingi wa magari tuliyonayo na uchache wa vyuo vya udereva tulio nao. Kuna wilaya na mikoa haina kabisa shule hizi na kwenye magari ya abiria na mizigo huko ndiyo kuna uhaba mkubwa," amesema Mkola. 


Amesema kuwa madereva wengi hawana vigezo lakini ilitokana na uhaba wa vyuo vya ufundishaji hivyo vijana wakawa wanatumia njia za mkato kupata leseni jambo alilosema kuwa kukosekana kwa mafunzo ndiyo kunafanya kuwepo na ajali nchi nzima ambazo zinatesa serikali jamii na Taifa 

"Sisi tuko vizuri tunatoa huduma kama  zinavyotolewa na hiki chuo hapa (ATC) sisi tunaenda kufundisha madereva wa kawaida, malori, mabasi na mitambo," anafafanua Mkola.


Kwa upande wake mkurugenzi wa shule  St Brian Driving School, Robert Mwinje, ameanza kwa kumpongeze Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya uwekezaji wa matrilioni ya fedha uiofanyika kwenye chuo cha ATC.

"Tumeona ujenzi wa mabweni ya kisasa, hospitali inayojengwa kwa ajili ya kumaliza changamoto ya huduma za afya ndani ya jamii ya wanaATC na tumeona maabara kwa ajili ya magari ya kisasa yale yanayotengenezwa nchini na yale yanayoagizwa nje ya nchi," Mwinje ameeleza na kufafanua zaidi.

...Uwekezaji wa shule za udereva ni mkubwa unahitaji rasilimali fedha na vitu  japo kuna vingine tumeona vilifunguliwa kwenye maeneo ambayo kuna shughuli nyingine zinaendelea na hiyo ikawakosesha sifa tunaamini watarekebisha ili waruhusiwe kuendelea".

"Jukumu ambalo ATC wamefanya limetunufaisha sana kwa sababu kulikuwa na uhaba wa wakufunzi ambapo ATC imezalisha wengi mwenzetu wakala wa Dar es Salaam ametoa wahitimu hivi karibunoina sisi Dodoma mafunzo yanaendelea," 

"Hiyo ndiyo ilikuwa changamoto kwa sababu unapozungumza ajali na kupambana nazo ni muhimu kuangalia vyanzo vyake kama hatuna waalimu wa kutisha ni hakika ajali zitaongezeka,".

 Mwinje amesema kuwa ATC inahitaji pongezi  kwa ubunifu huo wa kuzalisha waalimu wengi wa udereva wenye sifa "sisi kama mawakala tukitoka hapa ni kwenda kuitangaza ATC kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuzalisha  walimu wenye sifa na vigezo wa na ieleweke  walimu wakiwa hakuna wa kutosha kufundisha madereva basi ajali haziwezi kuisha ila kwa hawa wanaozalishwa kwa wingi tunaenda kupunguza ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva,".



 






0 Comments:

Post a Comment