WADAU wa sheria wametakiwa kuisaidia jamii kuelewa umuhimu wa kumaliza migogoro
kwa njia ya usuluhishi endapo si lazima kwenda mahakamani kwani
inapunguza uwezekano wa kutumia muda mwingi na rasilimali .
Hayo yameelezwa leo Januari 22, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela
wakati akizindua wiki ya sheria mkoani hapa kwenye viwanja vya TBA ambapo kauli
mbiu ni “Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza
uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau,”.
Amesema kuwa wananchi
watapata muda zaidi wa kujishughulisha kwenye shughuli za maendeleo badala ya
kuwa kwenye migogoro na kesi mahakamani.
Mongela amesema kuwa utatuzi
wa kesi kwa njia ya usuluhishi kwa kiasi kikubwa umesaidia wananchi kupata haki
zao na kuokoa muda mwingi.
"Tunategemea
mtaisadia jamii kuelewa zaidi faida ya usuluhishi wa migogoro na jinsi gani
mnaweza kusaidia kuondoa kutumia muda mwingi na rasilimali nyingi. Wakati
mwingine mgogoro kuisha kwa sheria huacha makovu natumaini dhana hii inaweza
kutusaidia sana," amesema Mongela na kuongeza
...Sisi tutategemea sana wiki hii itumike itoke kutoa elimu ya
kutosha...Hapa Arusha mhimili wa mahakama umekuwa na mchango mkubwa
sana. Unapoona utulivu wa mkoa wetu, tunapoona maendeleo makubwa kwenye
mkoa wetu mhimili wa mahakama una mchango mkubwa sana,".
"Niwapongeze wadau wote wa sheria, Haki inazidi kutendeka zaidi na hata
wananchi wanazidi kuona hivyo.Niombe mahakama kwa hatua tuliyofikia tuendelee na msimamo huo kusaidia
wananchi,".
“Mahakama ndiyo chombo pekee kilichopewa nguvu ya kutoa haki kwa mujibu wa
sheria.Sisi kama serikali tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwenu pale
panapohitajika,”
Mondela amesema kuwa sekta ya sheria inaweza kuchangia kudumisha amani na umoja
nchini huku akihimiza kauli mbiu ya maadhimisho hayo kutekelezwa na wadau wote
wa sheria.
“TLS (Chama Cha Wanasheria Tanganyika) wasaidie na nyie na wadau kutoa elimu muone jinsi mtakavyosaidia wiki hii mara nyingi watu
wakitoka kwenye wiki hii mashauri mengi huisha kutokana na elimu hiyo,”
alisisitiza Mongela.
Awali, Naibu Msajili Mahakama kuu Kanda ya Arusha, Judith Kamala amesema kuwa maadhisho
hayo ya wiki ya sheria yataaambatana na shughuli mbalimbali zitakazofanyika
ikiwemo kutoa elimu katika viwanja vya TBA, kutoa elimu kwa shule sita tofauti
zilizopo Arusha, gereza la mkoa la Kisongo na mahabusu ya watoto Arusha.
Aidha kutakuwa na hafla
ya kutembelea watoto wahitaji na kuwapatia msaada, bonanza litakalowashirikisha
wadau mbalimbali wa mahakama kutoka mikoa ya Manyara na Kilimanjaro.
Kilele cha maadhimisho
hayo ya wiki ya sheria inatarajiwa kuwa Februari mosi, 2023 ambapo yanatarajiwa
kufanyija kwenye a viwanja vya mahakama kuu.
Kwa upande wake, mwakilishi wa wakili wa serikali mfawidhi mkoani hapa, wakili Zamaradi Yohannes amesema
kuwa kama wadau wa haki watazingatia usuluhishi wa migogoro kwa njia ya utatuzi.
0 Comments:
Post a Comment