ACHPR WATUA NGORONGORO KUWASIKILIZA WANANCHI, VIONGOZI


SAKATA la mgogoro wa ardhi baina ya serikali na wananchi wa Ngorongoro limechukua sura mpya baada ya Tume ya Afrika ya binadamu na Haki za Watu (ACHPR) kuleta makamishna wawili nchini kwa ajili ya kuangazia hali ya haki za binadamu kwenye tarafa za Ngorongoro na Loliondo wilayani Ngorongoro.


Aidha, watetezi wa haki za binadamu wameiasa serikali kuona umuhimu wa kuikutanisha tume hiyo na wananchi na viongozi halisi wa Ngorongoro ili kuweza kupatia ufumbuzi mgogoro uliopo ambao umesababisha uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo watu kufa, wengine kujeruhiwa huku wengine wakipoteza mali.

Makamishina hao wamekuja kutokana na wito wa serikali ya Tanzania ambapo watakuwa nchini kwa siku tano kuanzia januari 23 mpaka 27 mwaka huu.

Makamishna hao ni  Mwenyekiti wa wanaosimamia haki za watu wa asili, (indigenous polulation and minorities), Litha Mustimi-Ogana  na mwingine, Ourvena Geereesga Topsy-Soono,  ambaye ndiyo anaisimamia Tanzania juu ya haki ya kujieleza na kupata taarifa.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha leo Januari 23, 2023 , Kamishna,  Litha amesema kuwa tayari wameshakutana na maafisa wa serikali na makundi ya watetezi wa haki ya binadamu na makundi ya jamii ya pembezoni hivyo wanaendelea kukutana na makundi mengine ya jamii.

Alisema kuwa ijumaa wiki hii Januari 27, 2023 watatoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukutana na wananchi,  viongozi wa serikali na wa kijamii wilayani Ngorongoro ambapo watakabidhi taarifa yao kwa serikali ya Tanzania na ACHPR.


Akizungumza  mara baada ya kukutana na makamishina hao Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa haki za Binadamu nchini,(THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa amesema kuwa lengo la ujio wa makamishna hao ni kuwasikiliza wananchi wenyewe hivyo ni vema serikali iwapeleke wakakutane na wananchi wenyewe,  madiwani viongozi wa vijiji vitongoji na viongozi wa mila wilayani Ngorongoro. 

"Wahakikishe wanakutana na viongozi halisi ili wakitoa mapendekezo yatusaidie sisi kama Taifa kwa lengo la kujenga," alisisitiza OleNgurumwa 


Akiongea kwa niaba ya watetezi wa haki za binadamu na wananchi wa Ngorongoro wanaoishi katika maisha ya kiasili, Ole Ngurumwa aliipongeza SCHPR kwa kutuma makamishna wake  kuja kufuatilia na kuwasililiza pamona na  serikali kwa kuwaalika.

 "Wamewaalika na kuwaruhusu kuja sehemu iliyokuwa na mzozano mkubwa kati ya serikali na wananchi ni uthubutu mkubwa kwa serikali kuruhusu tume iende ikaangaie," amesema OleNgurumwa.

Amesema kuwa jumanne Januari 24, 2023 makamishna hao walitarajia kuelekea Ngorongoro kwa ajili ya kukutana na wanajamii ambapo huko wanatarajia kukutana na kuongea na wahanga wa matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu yanayolalamikiwa kwenye tarafa za Ngorongoro na Loliondo.


"Kulikuwa na mvutano mkubwa kama Wamaasai kule ni watu wa asili tume hii haiendi kutoa tafsiri nani alikuwa wa kwanza kule au nani alikuwa wa mwisho," amesema OleNgurumwa na kuongeza 

...Kwa mujibu wa kamusi mtu wa asili ni mtu anayeishi maisha ya kitamaduni ni mtu anayetegemea mazingira yake ya kutamaduni kujiendesha kiasili bila kujali umekuja lini".

Amesema kuwa kwenye kikao chao na makamishina hao miongini mwa mambo ambayo waliyowaeleza ni kuwa taratibu za serikali kuchukua ardhi kilometa 1,500 kwenye tarafa ya Loliondo haukuwa shirikishi kuna malalamiko watu wameuawa, wameumizwa na kufunguliwa kesi mbalimbali.

Ole Ngurumwa amesema kuwa kwenye tarafa ya Ngorongoro watu wanahamishwa kwenda Mdomera wilayani Handeni mkoani Tanga bila kufuata utaratibu huku huduma muhimu  za kijamii kwa wananchi waliobaki zikiminywa hali inayowafanya waliobaki kuishi katika mazingira magumu.



Kwa upande wake mkazi wa Loliondo,  Nderango Laizer naye amesisitiza umuhimu wa makamishna hao wa ACHPR kukutanishwa na watu sahihi vinginevyo ufumbuzi wa mgogoro huo hautaweza kupatikana.


"Tume ikawasikilize watu halisia wa Ngorongoro na si wa kutengeneza kwa sababu kama tunataka kumaliza tatizo serikali ihakikishe inawakutanisha na watu halisia," amesema Laizer na kuongeza

...Watakaotoa taarifa sahihi hali ilivyokuwa kwenye matukio na wawatumie na viongozi halisi wa mila Malaigwanan ambao wao wenyewe wapo na watu pamoja na viongozi wa siasa hasa madiwani ambao wako kuke siku zote lengo tuweze kupata muafaka". 

Nderango aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapunduzi, (CCM) wilayani Ngorongoro ambaye alikamatwa  Juni mwaka jana pamoja na wananchi wengine 26 wa Loliondo na kuachiwa Januari 22, mwaka huu baada ya serikali kuwafutia kesi ya mauaji iliyokuwa ikiwakabili.

"Kwa kuja kwao tunaamini kuna mambo yatarekebishwa na inaweza kuja kuwa mkombozi kwa wananchi ingawa hakutaka kuingia kwa undani juu ya yale waliyowaeleza makamishna hao," amesema Nderango ambaye uenyekiti wake ulikoma baada ya kushindwa kushiriki uchaguzi uliofanyika yeye akiwa gerezani.






   

0 Comments:

Post a Comment