WAUMINI WA MADHEHEBU YA SHIA,WAADHIMISHA SIKU YA ASHURA KWA KULAANI MAUAJI YA IMAMU HUSEIN

WAUMINI wa madhehebu ya SHIA, mkoa wa Arusha,wameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein,mjukuu wa Mtume Muhamada S.A.W ,kwa kutoa tamko la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya maji,dawa, na damu kwenye hospitali mbalimbali,ili waweze kuishi maisha mazuri


Hayo yameelezwa Agosti 9, 2022 na Imamu mkuu wa msikiti wa Zahra mkoa wa Atusha, Shekhe Maulid Hussein Sombi,kwenye maadhimisho ya siku ya Ashura,ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu Husseini mjukuu wa Mtume Muhamada S.A.W, aliyeuliwa na mtawala dharimu, Yazid bin Muawiyah,kwenye mji wa Karbala,nchini, Iraq

Amesisitiza kuwa waumini wa dhehebu la SHIA ,hawataki kuona watu wanaishi katika ugomvi ,matusi bali waishi kwa amani na kupata huduma muhimu za kijamii "Sisi SHIA,tunamuunga mkono Rais Samia,katika juhudi zake za Kuleta maendeleo bila ya ubaguzi"alisema shekhe Maulid.

Amesema kuwa katika maadhimisho hayo ambayo yameanza Augosti mosi na yatafikia kilele chake Augosti 13,wamechangia chupa 58 za damu,ambazo tayari wameshazikabidhi kwa uongozi wa hospitali ya mkoa ya Mount Meru pia wametoa misaada ya vyakula na maji ya chupa kwa watu mbalimbali

Shekhe,Maulid,amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kupinga ukatili,manyanyaso ,uonevu kufanyiwa kwa mtu yeyote na badala yake kujenga upendo ,mshikamano na umoja bila ubaguzi na wanalaani tukio hilo lakuuliwa Imamu Hussein.

Kuhusu Sensa ya watu na makazi itakayofanyika Augosti 23 mwaka huu,amesema waumini wote wa dhehebu la Shia,mkoa wa Arusha,watashiriki kwa kuwa Sensa ina faida nyingi ambazo zinaiwezesha serikali kufahamu Idadi ya watu wake na kutoa huduma nzuri kulingana na mahitaji hivyo wao watashiriki kwenye Sensa.

Amesema bila Sensa serikali haiwezi kutekeleza mipango yake ipasavyo Sensa ni jambo la ,muhimu sana ili kuweze kupatikana kwa huduma bora zinazotosheleza lazima kolakitukufahamike idadi yake

Shekhe, Maulid,amesema Imam Hussein aliuliwa mwezi mtukufu wa Muharram,siku ya Ashura, akiwa na wafuasi 82 wakiwemo wanawake,watoto,Yatima na wajawazito tukio hilo la kikatili na kinyama, limekuwa ni la kihistoria hivyo wanabeba ujumbe wa mshikamano upendo na ushirikiano kuishi bila ubaguzi

Nae maalimu wa Chuo cha Ahlul bait centre,Sheikh Muhamad Hashim,amesema wanaadhimisha kifo cha mjukuu wa mtume Muhamad S.A.W ,Ikiwa ni hatua ya kuelewesha ulimwengu ubaya wa tukio hilo ili ukatili wa aina hiyo usije ukajirudia kwa wengine na. wanalaani tukio hilo








0 Comments:

Post a Comment