DK PIMA NA WENZAKE WAJIFUNIKA SURA, WAOMBA KESI YAO ISIKILIZWE

Washitakiwa wakiwa  Dk John Pima,Mariam (aliyebeba  Mtoto),Wakiwa mahakamani . 

 

KESI tatu za uhujumu uchumi zinazomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima, zimeahirishwa baada ya hakimu anayezikiliza kuwa na majukumu mengine.

 

Aidha, Wakili wa utetezi, Sabato Ngogo ameiomba mahakama hiyo kupangia tarehe ya mapema shauri hilo kwa kile alichoeleza kuwa imeaihirishwa mara tano mfululizo huku mteja wake akiwa na mtoto mchanga mahabusu kwenye gereza la Kisongo.

 

Mashauri hayo ambayo mawili yalikuwa wamekuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na moja kwa ajili ya kutajwa yameahirishwa leo, Agosti 11, 2022 na Hakimu Mkazi, Regina Oyier wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha mbele.

 

 Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule aliileza mahakama hiyo mashauri ya uhujumu uchumi namba 3/2022 na 4/2022 yalikuja mahakamani hapo kwa ajili kwa ajili ya usikilizwaji wa awali hivyo akaomba tarehe nyingine kwa ya kuendelea na hatua hiyo mbele ya hakimu anayesikiliza shauri hilo.

 

Alieleza mahakamani hapo kuwa shauri namba 5/2022 limekuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa hivyo akaomba tarehe nyingine ya kutajwa kwani bado wanaendelea na upelelezi.

 

 

Hakimu, Mh Mbelwa (Hakimu Mkazi Mfawidhi) ana majukumu mengine leo ndiyo sababu ya kuahirisha shauri hili,mtaendelea kusomewa hoja za awali Agosti 25, (baadaye tarehe ilibadilishwa na kuwa Agosti 18,2022).

 

 

Hata hivyo Mshitakiwa wa kwanza, Dk Pima alinyoosha mkono na kusimama kisha akamweleza hakimu, “Tulikuwa tunaomba tarehe iwe ya karibu zaidi kwa kesi zote mbili,” .

 

Wakili wa utetezi aliieleza mahakama hiyo wanaomba tarehe ya mapema kwani hii  ni mara ya tano usomaji huo wa maelezo ya awali (PH) shauri hilo linaahirishwa huku mshitakiwa mmoja, Mshana akiwa na mtoto mdogo mahabusu kwenye gereza la Kisongo.

 

Hiyo ilimfanya Hakimu Mkazi, Oyier alibadili tarehe ya awali iliyoangwa kwa ajili ya amashgauri hayo kurejea mahakamani hapo kutoka Agosti 25 mpaka Agosti 18, mwaka huu.

 

Katika shauri la uhujumu uchumi namba 4/20222 linalowakabili Dk Pima,Mariam,Maduhu na Alex Daniel.

 

Washitakiwa wengine ni pamoja na  aliyekuwa mkuu wa idara ya fedha ya halmashauri hiyo, Mariam Mshana (40), ambaye alikuwa amembeba mtoto wake mdogo mahakamani hapo na  aliyekuwa mkuu wa idara ya Uchumi na Mipango, Innocent Maduhu (40).

 

Shauri namba 5/2022 linawakabili  washitakiwa watano wakiwemo   waliokuwa wachumi katika jiji hilo, Nuru Ginana na Alex Daniel.

 

Awali, Juni 21, mwaka huu Dk Pima,Mariam,Maduhu na Alex Daniel walisomewa kesi Uhujumu uchumi yenye mashtaka sita yakiwemo  mawili ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana,


Mengine ni kutumia nyaraka kwa nia ya kumdanganya mwajiri ,ufujaji na ubadhirifu ambayo Dk Pima na wenzake walisomewambele ya hakimu Mkazi wa mahakama hiyo , Bittony Mwakisu anayesikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 5/2022.

 

 Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa sita ambapo kosa la kwanza linalowakabili ni ufujaji na ubadhirifu wa Sh103 milioni, kosa la pili na la tatu ni kutumia nyaraka kwa malengo ya kumdanganya mwajiri.

 

Kosa la tano linalomkabili Maduhu peke yake  ni utakatishaji fedha huku la sita likiwa ni la utakatishaji fedha linawakabili washitakiwa wote watatu.

 


 

Akiwasomea mashitaka hayo, Wakili wa Serikali, Kagilwa alieleza mahakamani hapo kuwa shitaka la kwanza linawakabili washitakiwa wote watatu ambapo ni la ufujaji na ubadhirifu kinyume cha sheria ya uhujumi uchumi na sheria za kuzuia na kupambana na rushwa.

 

 

Alidai mahakamani hapo kuwa  washitakiwa wote katika tarehe tofauti kati ya Machi 28, mwaka huu na April 14, mwaka huu wakiwa wameajiriwa wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wakiwa kama mkurugenzi wa halmashauri jiji la Arusha, Mkuu wa Idara ya Fedha na  mkuu wa Idara ya Uchumi na Mipango waliweza kutumia milioni 103 ambazo zimekuja kwao kupitia nafasi zao.

 

 

Wakili wa serikali Kagilwa alieleza kuwa  shitaka la pili linawakabili washitakawa wote watatu ambapo wanadaiwa  walituma  nyaraka kwa nia ya kumdanganya mwajiri wao kinyume cha sheria za kuzuia na kupambana na rushwa na uhujumi uchumi.

 

 

 

Alidai kuwa mnamo tarehe 27 machi mwaka huu katika jiji wilaya na mkoa wa Arusha washitakuwa hao  wakiwa wameajirikiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kutumia nyaraka, dokezo walitoa taarifa zao uongo kuonyesha kwamba Maduhu aliomba masurufu kwa ajili ya kununua mchanga moramu shilingi milioni 103 kwa nia ya kutengeneza matofali wakati wakijua ni uongo.

 

 

 

Katika kosa la tatu ilidaiwa mahakamani hapo kuwa  washitakiwa wote walitumia nyaraka kumdanganya mwajiri wao ambapo mnamo tarehe 27 machi, huu katika jiji wilaya na mkoa wa arusha kwa nafasi ya mkurugenzi  wa jiji la Arusha, Mkuu wa kitengo cha fedha na Mkuu wa  kitengo cha mipango na uchumi waliweza kumdanganya mwajiri.

 

 

 

Ilidaiwa waliandaa maombi ya masurufu ya safari zikiwa na taarifa za udanganyifu wakijifanya bwana, Innocent Maduhu ambaye ni mchumi aliomba malipo ya kiwanda cha ujenzi wa kiwanda cha matofali kiasi  cha shilingi milioni 103.

 

 

 

Ilidaiwa katika shitaka la nne washitakiwa hao walitumia nyaraka kwa nia ya kumdanganya mwajiri wao ambapo mnamo Aprili 28, mwaka huu walijifanya kuonyesha Maduhu alirejesha fedha za ununuaji 'material' kwa ajili ya ununuaji wa vifaa vya kujenga kiwanda cha matofali wakati wakijua si kweli.

 

 

 

Shitaka la tano la utakatishaji fedha linalomkabili, Madihu peke yake ambapo anadaiwa  mnamo Aprili , mwaka huu alijipatia gari yenye namba za usajili T 844 DYY aina ya Subaru Forester kwa fedha ambazo ni zao la uhalifu la  kumdanganya mwajiri wake

 

 

 

Wakili Kagilwa alisoma shitaka la sita la utakatishaji fedha linalowakabili washitakiwa wote watatu   wanadaiwa kuwa katika terehe tofauti kati ya Machi 23, mwaka huu na Mei 25, mwaka huu walijipatia fedha taslim sh milioni 103 wakati wakijua fedha hizo zilitokana na zao la uhalifu la kumdanganya mwajiri wao.

 

 

 

 

 

Awali Juni 17, mwaka huu, Dk Pima na wenzake wanne walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Bittony Mwakisu, wakikabiliwa na makosa nane katika kesi mbili za uhujumu uchumi.

 

 

Dk Pima na wenzake watatu Innocent Maduhu (aliyekuwa mchumi wa Jiji), Nuru Ginana (mchumi), Alex Daniel (mchumi), 

 

 

 

 

 

Katika kesi ya kwanza,  Dk Pima, Mariam, Maduhu na Ginana wanakabiliwa na mashitaka manne ambayo ni ufujaji na ubadhirifu huku makosa mengine yakiwa ni matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri.

 

 

 

Awali katika kesi ya kwanza ya uhujumu uchumi namba 3/2022 inawakabili Dk Pima,Mariam,Maduhu na Ginana wanakabiliwa na mashitaka manne ambayo ni ufujaji na ubadhirifu huku makosa mengine yakiwa ni matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri.

 

 

Kosa la kwanza ni ufujaji na ubadhirifu ambapo kwa pamoja wanadaiwa kati ya Aprili 14 hadi 16 mwaka huu,katika wilaya na Mkoa wa Arusha wakiwa waajiriwa wa serikali,walitenda  kosa la ufujaji na ubadhirifu wa fedha  Sh67 milioni.

 

 

Shitaka la pili ni matumizi ya nyaraka kwa malengo la kumdanganya mwajiri ambapo wanadaiwa kutumia nyaraka iliyokuwa na kichwa cha habari dokezo lenye maelezo kuwa Nuru amenunua na kusambaza moramu yenye thamani ya Sh65 milioni kwa ajili ya Soko la Samunge huku wakijua nyaraka hiyo siyo ya kweli na wakimdanganya mwajiri.

 

 

 

Shitaka la tatu ilidaiwa kuwa ni matumizi ya nyaraka kwa malengo ya kumdanganya mwajiri,ambapo wanadaiwa Aprili 14,2022 wakiwa na nia ovu walitumia nyaraka ya maombi ya masurufu(safari) ikionyesha Nuri amenunua na kusambaza moramu ya Sh65 milioni huku wakijua wanamdanganya mwajiri wao.

 

 

Alitaja shitaka la nne kuwa ni matumizi mabaya ya nyaraka kwa malengo ya kumdangaya mwajiri ambapo wanadaiwa Aprili 28,mwaka huu wakiwa na nia ovu ua kumdanganya mwajiri walitumia nyaraka ya marejesho ya masurufu ikionyesha Nuru amefanya marejesho ya Sh65 milioni ikiwa ni malipo maalum ya  kazi za nje ya kituo chake cha kazi.

 

 

 

Katika kesi ya pili ya uhujumu uchumi namba 4/2022 washitakiwa ni Dk Pima,Mariam,Maduhu na Daniel wanakabiliwa na makosa manne ikiwemo la ufujaji na ubadhirifu pamoja na matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri.

 

 

Akiwasomea mashtaka hayo,Wakili Akisa alidai kosa la kwanza ni ufujaji na ubadhirifu ambapo kati ya Aprili 14 hadi 16,mwaka huu wakiwa waajiriwa wa serikali kwa pamoja na kwa nia ovu walifanya ufujaji na ubadhirifu wa fedha za umma kwa matumizi yao binafsi Sh65 milioni iliyokuwa imetolewa kwa ajili ya matumizi ya umma.

 

 

Alitaja shitaka la pili katika kesi hiyo kuwa ni matumizi ya nyaraka kwa malengo ya kumdanganya mwajiri kinyume na sheria ambapo wanadaiwa Aprili 14,mwaka huu walimdanganya mwajiri kupitia nyaraka yenye dokezo lililokuwa linahusiana na shughuli za kila siku za mwajiri ambapo walidanganya Daniel amenunua na kusambaza moramu yenye thamani ya Sh65 milioni huku wakijua kwa kufanya hivyo ni kumdanganywa mwajiri.

 

 

 

Alidai shitaka la tatu kuwa ni matumizi ya nyaraka kwa malengo ya kumdanganya mwajiri ambapo,Aprili 14,mwaka juu wakiwa na nia ovu walitumia nyaraka ya maombi ya masurufu,ikiwa na maelezo ya uongo yakionyesha Daniel amesambaza moramu kwa ajili ya matengenezo ya barabara hivyo adai Shilingi 65 milioni huku wakijua wanamdanganya mwajiri wao.

 

 

Shitaka la nne ni matumizi ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri ambapo wanadaiwa kwa pamoja wakiwa na nia ovu kupitia nyaraka iliyokuwa na kichwa cha habari marejesho ya masurufu iliyoandikwa Aprili 26,2022 iliyohusiana na shughuli za mwajiri.

 

 

Alidai nyaraka hiyo ilikuwa na maelezo ya udanganyifu kuwa Alex anafanya marejesho ya Shilingi 65 milioni ikiwa ni matumizi ya kusambaza moramu katika taasisi mbalimbali za serikali kwa ajili ya kutengeneza barabara huku wakijua kwa kufanya hivyo wanamdanganya mwajiri.

 

 

 


 

 


0 Comments:

Post a Comment