PROF NDAKIDEMI ATAKA VIJANA KUJIKITA KWENYE KILIMO

 

 Na Gift Mongi

Moshi

Vijana  mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuchangamkia  fursa za kilimo kwa kulima mazao ya kibiashara  ambayo  itawawezesha kujikwamua kiuchumi tofauti na kufanya kazi hiyo kimazoea.



Hayo yamebainishwa na mbunge wa Moshi Vijijini   Prof, Patrick Ndakidemi wakati alipokuwa akizungumza katika kongamano la  vijana la kuwahamasisha  kujikita katika kilimo biashara iliyofanyika mkoani  Kilimanjaro.


Amesema kuwa Wizara ya kilimo imetenga  fedha ya kuwasaidia vijana waliojikita katika kilimo,na kusema ni vyema vijana  wakajiunga katika vikundi  ili waweze kupatiwa fedha hizo na waweze kuondokana na tatizo la umasikini.


"Vijana ambao wamehamua kufanya sekta ya kilimo kama ajira na kulima kwa mfumo wa kilimo biashara, wamekiri kupata mafanikio makubwa tofauti na ajira ambazo walikuwa nazo hapo awali"Amesema Prof.Ndakidemi.


Sambamba na hayo amelipongeza kanisa la KKKT kupitia shirika la Norwegian Church Aid  kwa kuwaleta vijana hao pamoja ili waweze kuelezea mambo mbalimbali ya kimaendeleo wanazofanya na kusema jambo Hilo ni muhimu na lina Maendeleo kwa Taifa.


Amewataka pia vijana kujitambua na kujua thamani walizonazo kwani wao ndio taifa la leo na taifa la kesho ambapo amesema vijana walio wengi hawajielewi hivyo amewataka kujitambua hata kama hawana ajira lakini wanaweza kujiiingiza katika fursa za kilimo.


Hata hivyo amesema kama vijana watatumia karama walizonazo na kujingiza kwenye ujasiriamali wataaweza kufanikiwa bila kutegemea kuajiriwa mahali popote.


Martin Mshiu miongoni mwa vijana mjini Moshi amesema kuwa fursa ya kilimo ni nzuri katika kuwakwamua vijana kiuchumi lakini tatizo ni mtaji kwani kilimo kinahitaji uwekezaji wa fedha ambazo vijana hawana.


"Sisi tunakabiliwa na changamoto ya kupata mitaji ila zikijitokeza fursa sidhani kama kuna kijana ambaye atakataa kujihisisha na kilimo kwani ni biashara yenye uhakika"amesema



0 Comments:

Post a Comment