RUFAA YA SHERIA YA VYAMA VINGI, EACA YAMPA AG WA TANZANIA SIKU 14



MAHAKAMA ya rufaa ya Haki ya Afrika Mashariki, (EACA), imempa siku 14 mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, (AG) kufanyia marekebisho nyaraka za rufaa walizosiwasilisha baada ya kuonekana zinapungufu kisheria.

Rufaa hiyo inapinga uamuzi ulitolewa na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, (EACJ) Machi 25, mwaka huu ukiiamuru serikali ya Tanzania kurekebisha Sheria ya vyama vya siasa, ili iondoe vifungu vinavyokiuka makataba ulioianzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC) ambapo  hukumu iliyotolewa kuhusu kesi iliyofunguliwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake sita.

Amri hiyo imetolewa leo Agost 9,2022 na Rais wa Mahakama Rufaa, Jaji, Nestor Kayobera anayeongoza jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo , akiwemo majaji, Sauda Mjasiri na Anitha Mugeni.

Shauri hilo la rufaa namba 5/2022 lilikuwa limefika mahakamani hapo kwa ajili ya kupanga utaratibu wa namna ya kulisikiliza ambapo mawakili wa pande zote wangekubaliana endapo litasikilizwa kwa njia ya mdomo au maandishi.

Pia wangepanga tarehe ya waleta rufaa kuwasilisha hoja zao na siku ya wajibu rufaa kuleta hoja zao za majibu kisha upande wa waleta rufaa kuwasilisha hoja za ziada endapo wataona ni vema kufanya hivyo kisha mahakama itakaa  ipange siku ya kusoma hukumu.

Hata hivyo mara baada ya mahakama hiyo kuanza jaji, Kayobera alieleza kuwa kulikuwa hakuna ukurasa unaoonyesha yaliyomo ndani ya rufaa hiyo (index) kwenye nyaraka za rufaa zilizowasilishwa na upande wa jamhuri ambayo kwa mujibu wa kanuni 99 za uendeshaji wa mashauri wa mahakama hiyo ni lazima iwepo .

Upande wa Jamhuri kuwasilisha nyaraka hizo za rufaa mara mbili tofauti mwezi April na Mei lakini zote hazionyeshi ukurasa huo wa 'index'.


Hata hivyo, Rais huyo wa mahakama hiyo alienda mbele zaidi kwa kueleza kuwa kanuni ya 100 ya uendeshaji mashauri kwenye mahakama hiyo unatoa fursa ya kuweza kufanyia mabadiliko nyaraka hizo endapo shauri hilo bado halijapangiwa utaratibu wa namna ya kulisikiliza.



Kwenye shauri hilo upande wa waleta rufaa unawakilishwa na Mawakili wa Serikali, Narindwa Sekimanga, Charles Mtae na Zamarad Johanes huku upande wa wajibu rufaa ukiwasilishwa na mawakili, John Mallya, Jebra Kambole na Ditto Amre. 



"Attorney General aliapaswa kuleta maombi hayo ya kufanya marekebisho yakiwa na 'index' lakini kwa maslahi ya haki tumefanya haya ili maombi haya  yakidhi  matakwa ya mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo," alieleza jaji Kayobera.

Wakili wa Jamhuri, Sekimanga aliomba wafanye marekebisho hayo bila gharama ambapo aliomba mpaka ijumaa Agosti 12, mwaka huu watakuwa wamewasilisha upya mahakamani hapo kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 99.

Wakili wa wajibu rufaa, Mallya alisema hawana pingamizi na mabadiliko hayo ila wakautaka upande wa jamhuri kuhahakikisha wanakamilisha taratibu hizo kama walivyoelekezwa ili shauri hilo liweze kuendelea.

Hata hivyo Jaji, Kayobera aliwapa siku 14 mawakili hao wa serikali kuwa wamewasilisha marekebisho hayo kwenye rufaa hiyo wakizingatia kanuni ya 99 inavyoelekeza juu uwasilishaji wa mashauri ya rufaa mahakamani hapo.


" Tunaomba 'Attorney General' (mwanasheria mkuu wa serikali) achukulie hili ni kawaida ila tunataka kuhakikisha  kanuni za uendeshauri ya mahakama hii zinafuatwa ili kuhakikisha haki inapatikana," alisisitiza Jaji Kayobera wakati akiahirisha shauri hilo.

Mara baada ya mawakili wa upande wa waleta rufaa kuwasilisha mabadiliko hayo mahakamani haoo Agosti 23, mwaka huu mahakama hiyo itapanga siku ya kuita oande zote kwa ajiki ya kuoanga utaratibu wa kusikiliza shauri hilo.

Awali Machi 25, mwwka huu kwenye mahakama yq EACJ ilisema kuwa sheria hiyo inakiuka vifungu vya mkataba wa wa kuanzishwa EAC.


Sheria hiyo ambayo ilitiwa saini na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano , John Pombe Magufuli mwezi Februari mwaka 2019 na kuchapishwa katika gazeti la serikali siku 10.



0 Comments:

Post a Comment