Hayo yamejiri leo wakati shahidi huyo akihojiwa maswali ya dodoso na wakili wa Serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza shauri hilo namba 27/2021 kwenye mahakama ya hakimu Mkazi Arusha.
Odemba ambaye pia ni mshitakiwa wa nne kwenye shauri hilo alimwambia wakili huyo hivyo ambaye alitaka kujua sababu za yeye kumwaga machozi mahakamani inatokana na yeye kujutia makosa yake akamjibu usiniulize kuhusu kulia kwangu kwani wewe unaonaje.
Shahidi aliendelea kuieleza mahakama kuwa hajui anakuja lini jijini Arusha ila ni zaidi ya miaka nane huku akisistiza kuwa hakumbuki mwaka halisi ambapo wakati wakili Mtenga akiendelea kumbana juu ya swali hilo ghafla wakili wake, Moses Mahuna alisimama akamuombea ruhusa ya kwenye chooni.
Hakimu aliridhia huku akimuuliza wakili huyo mbona shahidi hajaomba kisha ghafla mshitakiwa wa kwanza, Sabaya naye akasimama akielekea mlangoni jambo lilimfanya hakimu kuhoji kwani uliomba ruhusa kwa ajili ya mshitakiwa yupi ambapo wakili, Mahuna alisema ni Odemba ila nadhani na Sabaya naye alikuwa anahitaji.
Baada ya shahidi huyo kurejea, aliendelea kujibu maswali ya Dodoso ya wakili, Mtenga ambapo alieleza kuwa yeye alikuwa mfanyabiashara wa nguo za mtumba akiwa na mtaji wa milioni tatu lakini hana leseni wala namna ya mlipa kodi, (TIN) isipokuwa ana kitambulisho cha mjariamali.
Odemba alieleza mahakamani hapo kuwa anafanya biashara hiyo kwenye kibanda alichojenga kwenye kiwanja cha mtu asiyemjua huku akimuuliza wakili Mtenga anataka amtaje jina huyo mtu kwani anamjua?.
Hata hivyo amesema hawezi kuleta kitambulidho hicho cha Mjasiriamali mahakamani hapo ambacho hakina jina lake ila namna tu kwani kipo kwa wakili wake, Fridolini Bwemelo ambaye hakuwepo mahakamani hapo leo.
Odemba alieleza kuwa alikutana na maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, (TAKUKURU) akiwa mahabusu kwenye gereza Kuu la Kisongo ingawa mara ya pili hawakuweza kuzungumza nao baada ya kushindwa kuelewana hivyo bwana jela msaidizi akawafunguza.
Hata hivyo alisema hayuko tayari kumleta bwana jela msaidizi wala askari magereza waliosikia mazungumzo baina yao na maafisa hao wa TAKUKURU licha yankuwa anawafahamu na wapo kwenye gereza hilo kwani hawahusiki na kesi hivyo akaitaka mahakama kuamini maneno yake aliyoyatoa chini ya kiapo.
Sehemu ya mahojiano mahakamani hapo wakati wakili wa serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga akimuuliza shahidi, Odemba maswali ya dodoso
Wakili: Bwana Odemba mbona unalia unajuta ?
Shahidi; Wewe unaona nini
Wakili; Nakuuliza kujua
Shahidi; usiniulize kulia kwangu
Wakili; umesema unaishi wapi
Shahidi; Njiro Arusha
Wakili; Umesema umeishi Arusha miaka nane
Shahidi; Zaidi ya miaka nane
Wakili: Ulikuja lini Arusha
Shahidi; Sikumbuki siku wala mwaka ila zaidi ya miaka nane
Wakili; Wewe umesoma
Shahidi; Ndiyo
Wakili; Mpaka la ngapi
Shahidi; la saba
Wakili; Wapi kwingine umewahi kuishi
Shahidi; Bukoba, Dar es Salaam na Arusha
Wakili; Na haujui Arusha ulikuja lini
Shahidi; zaidi ya miaka nane nyuma
Wakili; Mwaka gani
Shahidi; zaidi ya miaka nane nyuma
Wakili; unauzia mitumba kwenye nyumba ya nani.
Shahidi Nimejenga kibanda
Wakili; Kwenye kiwanja cha nani
Shahidi; Pale ninapoishi, kwenye sehemu ninapoishi nimeomba sehemu nikajenga kibanda
Wakili; Nitajie jina la huyo mtu
Shahidi; nikutajie huyo mtu unamjua? simjui jina
Wakili; Na Njiro unakaa kwenye
nyumba ya nani?
Shahidi; Niko kwangu
Wakili; Kwenye nyumba ya kwako plot
namba ngapi
Shahidi; Sijapata namba ya kiwanja
Wakili; Hizo nguo zako unazouza huwa
unachukua wapi?
Shahidi; Tengeru krokoni na Moshi
Wakili; Una leseni kwenye biashara
zako hizo
Shahidi; Ninayo
Wakili; Unayo TIN
Shahidi; Nina kitambulisho cha
mjasiriamali mdogo
Wakili; Kiko wapi
Shahidi; Anacho wakili wangu Gwemelo
Wakili; Mtaji wako ni mkubwa kiasi
gani
Shahidi; Milioni 3
Wakili; Unataka kuongea na wenzako
naona unachezesha mdomo
Shahidi; Naongea nao nini
0 Comments:
Post a Comment