Na Gift Mongi,Moshi
VIJIJI sita vilivyopo katika kata ya Kimochi halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro vinatarajiwa kunufaika na mradi wa maji safi na salama jambo lililoelezwa litaenda kupunguza kero za kutembea umbali mrefu wa kutafuta huduma hiyo.
Prof Patrick Ndakidemi ni Mbunge wa jumbo la Moshi Vijijini ambapo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji kwenye kata hiyo ya Kimochi na kueleza kuwa serikali ina nia ya kuondoa kero ambazo ni sugu kwenye jamii.
Prof Ndakidemi aliongozana na diwani wa kata hiyo Ally Badi, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini Ramadhan Mahanyu na Mkurugenzi wa MUWSA Mhandisi Kija Limbe pamoja na watendaji wa MUWSA alisema changamoto za mahi katika jumbo hilo zimeendelea kutatuliwa ka awamu na kuwa muda mchache ujao suala hilo litabaki historia
"Hapa vijiji sita vinaenda kunufaika muone ambavyo serikali inawajali wananchi wake lakini mradi huu ni muhimu kwani unahudumia wananchi wa vijiji vya Shia, Sango, Mdawi, Mowo, Lyakombila na Kisaseni." Alisema
Kwa mujibu wa Prof Ndakidemi ni kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejizatiti katika kuhakikisha kuwa inamaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama linalowakabili wananchi.
"Niishukuru serikali inayoongozwa na rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za kutatua kero ya maji na miradi mingine iliyopo kwenye Kata ya Kimochi ukiwepo mradi wa ujenzi wa madarasa (5) katika shule ya Sekondari Kimochi yenye thamani ya Shilingi milioni 100 ambazo zilitolewa fedha za UVIKO 19" alisema Prof Ndakidemi.
Alisema kuwa mradi mwingine mkubwa ni ule wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri ya Moshi huko Sango uliopatiwa kiasi cha shilingi milioni 979,277,342.
Mkurugenzi wa Muwsa, Mhandisi Kija Limbe alieleza kuwa mradi huo wenye thamani ya Tsh milioni 500 unagharamiwa na fedha za UVIKO 19 na unatekelezwa na MUWSA na unategewewa kutatua kero ya uhaba wa maji inayowakabili wananchi waliopo eneo la mradi.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Ally Badi alimshukuru mbunge kwa ushirikiano mkubwa uliopo pamoja na kuwashukuru watendaji wote wa MUWSA kwa kazi kubwa wanayofanya katika kata hiyo kuwapatia wananchi maji katika maeneo yao.
0 Comments:
Post a Comment