Akizungumza leo Jumapili katika Kanisa Kuu la Azania Front wakati wa ibada ya shukrani, leo Machi 6, 2022 Mbowe amesema kuwa watu wengi walikuwa wanaomba mara kwa mara kuwa kesi hiyo ifutwe lakini yeye alikuwa anaomba isifutwe hadi ukweli ujulikane.
Kesi hiyo ilifutwa Ijumaa Machi 4, 2022 baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo ikiwa zimepita siku 216 tangu kuanza kusikilizwa kuanzia Jumanne ya Agosti 31, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Mbowe amefutiwa mashtaka baada ya kukaa gerezani siku 227 akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Februari 18, 2022, Jaji Joachim Tiganga aliyrkuwa anasikiliza shauri hilo lililokuwa likifuatiliwa na wengi ndani na nje ya nchi alitoa uamuzi kwamba Mbowe na wenzake watatu - Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohammed Ling’wenya wana kesi ya kujibu, hivyo kutakiwa kuanza kujitetea kuanzia Machi 4, 2022.
0 Comments:
Post a Comment