SAMIA ATAKA BENKI KUFUNGUA MATAWI NJE YA MIPAKA


Benki za Biashara nchini zimehimizwa kuchangamkia fursa ya kufungua matawi katika nchi za nje hivyo kuendelea kushindana vilivyo na benki nyingine kubwa.

RaisSamia Suluhu amezimbia benki hizo kuwa anafarijika kuona benki za nchi yake zinakuwa na uwezo wa kushindana na benki nyingine za nje na kwamba anapenda kuona sekta ya benki ambayo ni kubwa imara, shindani na inayokua siku hadi siku.

‘Nawatia moyo endeni kote inapowezekana nje… wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini, wao wana kili na sisi tuna akili’ Amesema Rais Samia.

Ameyasema hayo leo Machi 5, 2022 wakati akizindua jengo la makao mkuu ya benki ya CRDB ambayo ni moja ya kubwa za kibiashara nchini Tanzania huku akimwagiza mwenyekiti wa chama cha mabenki Tanzania kuungana kutekelza shabaha hiyo.

Ingawa hakufafanua ila kauli ya Rais inaonesha anapenda benki za Tanzania kutanua mtandao wake kwenda nchi nyingi ikiwemo zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingine Afrika, na duniani kama zilivyo benki nyingine za nje zenye matawi Tanzania.

CRDB ndiyo benki ya Tanzania yenye tawi nchini Burundi na inapanga kujitanua hadi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Baadhi ya benki za Afrika Mashariki zenye matawi Tanzania ni Kenya Commercial Bank (KCB) na Equity Bank pia ya Kenya. Nje ya Afrika Mashariki benki za kiafrika zenye matawi Tanzania ni pamoja na ABSA ya Afrika Kusini na BankABC ya Zimbabwe.


0 Comments:

Post a Comment