Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema hana nia ya kuweka sheria ya kijeshi nchini kwake, lakini akatahadharisha kuwa nchi yoyote ambayo itaweka "no-fly zone' juu ya anga ya Ukraine itachukuliwa kama imejiunga na vita nchini Ukraine.
"Kusogea kokote katika mwelekeo huu kutachukuliwa na sisi kama kushiriki katika mzozo wa silaha nan chi hiyo ," rais wa Urusi anasema.
atika dhana ya kijeshi,no-fly zone ni eneo ambako ndege zimewekwa marufuku ya kuingia ili kuzuwia mashambulizi au upelelezi. Lakini lazima itekelezwe kwa njia ya kijeshi- ikimaanisha , kunakuwa na uwezekano wa kudungua ndege.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameilaumu Nato kwa kushindwa kuwekano-fly zone Nato akisema ni "udhaifu’’ na ‘’ukosefu wa umoja".
Nato imesema kwa kufanya hivyo itasababisha vita kuwa vibaya zaidi kwa nchi nyingine nyingi zaidi
0 Comments:
Post a Comment