MOTO ULIVYOTEKETEZA KIWANDA CHA GSM


KIWANDA kutengeneza magodoro kinachomilikiwa na Kampuni ya GSM kilichopo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam kimeteketezwa na m
oto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzimwa kwa moto huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto Kinondoni, Christina Sungwa amesema wamepokea taarifa ya tukio hilo leo Jumapili Machi 13, 2022, majira ya asubuhi 12:50.


"Baada ya kupata taarifa hiyo tulifika haraka eneo la tukio, tukaomba msaada kwa wenzetu wa bandari na kampuni binafsi wanaohusika na shughuli za uzimaji moto", amesema Sunga.

Amesema hakuna taarifa yeyote ya majeruhi na mpaka sasa bado thamani halisi ya hasara iliyopatikana kutokana na tukio hilo bado haijajulikana.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema moto huo umedhibitiwa na haujaleta madhara makubwa.

0 Comments:

Post a Comment