MAWAKILI WA PANDE ZOTE KESI YA SABAYA, WAMKOMALIA SHAHIDI ALIYESHINDWA KUTOA USHAHIDI KISA SIMU


MSHITAKIWA wa tatu, Watson Mwahomange kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili pamoja na Lengai Ole Sabaya  ameibua manishano ya kisheria mahakamani baada ya kuiomba manakama iiamutu taasisi ya kuzuia na kupambana  na Rushwa, (TAKUKURU) impatie simu yake aweze kuitumia kujitetea.



Mwahomange ambaye anajitetea mwenyewe baada ya wakili wake kujitoa aliyoa ombi hilo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisonda anayesikiliza shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27/2021 kwenye mahakama ya hakimu Mkazi Arusha.

Ameeleza kuwa simu hiyo ipo miongoni mwa vielelezo ambavyo mawakili wa utetezi walipanga kuvitumia mahakamani hapo.


"Nilikuwa naomba mahakama yako iiamuru TAKUKURU  walete simu yangu ili nitumie kama kielelezo kwenye ushahidi wangu," ameomba Mwahomange mahakamani hapo.


Wakili wa serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga alipinga maombi hayo kwa kile alichoeleza kuwa Shahidi huyo anapaswa kuwasiliana na TAKUKURU bila kuihusisha mahakama. 


"Mheshimiwa hiyo ni juu yake yeye kufanya mawasilaino na TAKUKURU kwa njia ya barua au vinginevyo lakini kutaka mahakama iamuru haiwezekani hivyo awasiliane na TAKUKURU yeye mwenyewe," amesema Mtenga.

Mawakili wa utetezi wakaungana na mawakili wa Jamhuri kupinga mahakama kutoa amri hiyo ambapo wakili, Moses 
Mahuna alimtaka shahidi huyo kufuata taratibu aipste simu hiyo na si kuitumia mahakama kama basi la kumbeba.

" Kwa upande wa mshitakiwa  wa kwanza na wa pili,  tunapinga ombi hilo kwa sababu mahakama hii siyo sehemu ya mwenendo.  Shauri hili siyo la madai, kuitaka mahakama ikaingie kwenye process ya seinzing vielelezo ili vitumike kama ushahidi hiyo procedure ni mpya," amesema Mahuna na kuongeza

....Tunaungana na wakili Mtenga alichokisema kesi ni ya kwake mahakama haifahamu hata kama ana simu, haijui kama iko TAKUKURU kwa hiyo simu yake kokote ulIpo akaitafute mwenyewe aje nayo hapa atajua atakavyojenga ushahidi wake.


...Lakino sio kutumia mahakama kama basi la kumbeba kwenda kufanikisha analotaka,".


Wakili, Edmund Ngemela anayewawakilisha mshitakiwa wa nne na wa saba  amesema anaungana mkono  hoja za mawawakili wa Jamhuri.

" Tunaungana na mawakili hasa wa Jamhuri tunaungana anaye alichokisema. Mheshimiwa kama kweli simu ingekuwa imechukuliwa na TAKUKURU  na ninavYofahamu taratibu zA sheria huwa wanachukua kwa kutumia fomu maalum," ameeleza Ngemela na kuongeza


...Hata mahakama ikisema iletwe hakuna ushahidi  hapa mahakaman unaoonyesha simu ya mshitakiwa namba tatu ilikuwa siezed na Takukuru.


....Kuamuru simu iletwe wakati hatujui simu ni ya aina gani na ina imei namba ngapi, simu yoyote inaweza kuletwa na jamhuri kama amri yako utatoa simu yoyote inaweza kuletwa hapa mahakamani ambayo hatujui kama ndiyo yenyewe.


...Shauri limeanza muda kidogo ni rai yetu kama mshtakiwa wa tati alikuwa anataka kufanya hivyo angetoa taarifa mapema, mahakama haina uwezo wa kutoa amri kuruhusu kileleezo ambavyo hata hakikijui.


...Kwa misingi hiyo tunaomba mahakama yako tukufu izingatie hoja zetu imkataze kwa nguvu zote,".

Hata hivyo mshitakiwa huyo wa tatu, Mwahomange alipinga hoja za mawakili hao kwa madai kuwa hazina mashiko.

"Mheshimiwa hakimu nilikua naomba mahakama ipinge hoja ya wakili ngemela na mahuna kwa kuwa hazina mashiko yoyote. Nilikamatwa na TAKUKURU  wakawa na simu yangu, niko gerezani walichukua simu yangu,"  amesema Mwahomange na kuongeza.

... Pia mheshimiwa hakimu wakili Mahuna alisema tutakuwa na vielelezo vingi sana. Simu yangu nilikuwa naomba iwe simu yangu, kwa kuwa wakili  amejitoa naomba nitumie kama kielelezo,".


Hakimu: Vile vielelezo vilivyotajwa na Mahuna moja wapo ni hiyo simu?


Mwahomange; Ndiyo mheshimiwa hakimu, hivyo ilikua naiomba mahakama yako ifanye maamuzi



Hakimu; Nitatoa maamuzi kuhusu maombi ya mshitakiwa wa namba tatu lakini kama sijafanya hivyo hataweza kujitetea kesho nitatoa maamuzi.Kama kuna washitakiwa wengine wanaweza kuendelea kujitetea

0 Comments:

Post a Comment