Na Arodia Peter ,Unguja
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema kufanya Mkutano mkuu maalum kwa ufadhili ya wanachama wa chama hicho ni salamu tosha kwa wapinzani wao.
Amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) walidhani kuwa baada ya uchaguzi Mkuu wa 2020 Wazanzibar watavunjika moyo kutokana na hila, lakini badala yake wamezidi kuwa na hamasa na utayari wa kuitafuta Zanzibar yenye mamlaka kamili.
Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, aliyasema hayo leocMachi 13, 2022 huko Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, alipotembelea na kuzungumza na wanachama wa Barza ya vijana ya ‘Marhaba’ katika mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama kwa majimbo ya Zanzibar.
Othman alisema kitendo cha wanachama wa ACT Wazalendo kuweza kuchagia na kuhakikisha unafanyika mkutano mkuu maalum na kukamilisha safu ya viongozi ni hatua kubwa na ya utayari katika kuipigania Demokrasia na mamlaka kamili ya Zanzibar.
"Sisi tunaongozwa na dhamira ambayo ni kuyatafuta mamlaka kamili ya Zanzibar hivyo hatuwezi kurudi nyuma kwa vitimbi vyao" alisema Othman.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Ismail Jussa katika salamu zake kwa wanabarza hao alisema, Zanzibar iliyokuwa Dola kamili yenye kujitegemea sambamba na kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa imepoteza hadhi hiyo na badala yake imekuwa mshirika wa muungano na kukosa maslahi yake makubwa kama ilivyokuwa awali.
Akisisitiza katika hilo, Jusa alisema, ACT Wazalendo hakiukatai Muungano, isipokuwa ni muhimu kuwa na muungano wa haki na usawa kwa kila upande na wenye kuheshimika.
Akisoma risala mwanachama wa Barza hio ya vijana ya Marhaba, Yusuf Saleh Ali, amesema wameamua kuanzisha barza hiyo kwa lengo la kuelimisha vijana na umma wa Wazanzibari katika kuyapigania maslahi ya nchi yao.
Katika ziara hiyo, othman aliambatana na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salim Biman pamoja na Mshauri wa chama Juma Said Sanani.
Wajumbe wengine kwenye ziara hiyo ni wale wa kamati kuu, ngome za Wazee, Wanawake.
0 Comments:
Post a Comment