MAWAKILI wa Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili kuwasilisha hoja 14 za rufaa ambapo wamedai hakimu aliyetoa uamuzi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha alishindwa kufanya uchambuzi wa ushahidi na mashahidi hivyo akatoa hukumu ambayo haikuwastahili.
Aidha, wamedai polisi hawakufanya upelelezi wao vizuri huku ndiyo sababu hawakuweza kubaini malalamiko ya shahidi wa sita, Bakari Msangi yaliyokana na tofauti zake na Sabaya wakati akiwa UV CCM na hakupenda alipoteuliwa kuwa DC wa Hai.
Hayo yameelezwa leo Februari 15,2022 kwa nyakati tofauti na mawakili wa mleta maombi wa kwanza Sabaya, Majura Magafu na Moses Mahuna wakati wakiwasilisha hoja zao za rufaa mbele ya jaji, Sekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma anayesikiliza shauri hilo kwenye mahakama kuu kanda ya Arusha.
Kwenye rufaa hiyo wanapinga hukumu iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi Arusha ambapo Sabaya na wenzake Silvester Nyengu na Daniel Mbura walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kutengeneza genge la uhalifu.
Wakili Magafu aliieleza mahakama hiyo kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 312 cha uendeshaji mashauri ya jinai, (CPA) sheria inataka jaji au hakimu anapoandika hukumu yake inabidi afanye mchanganuo wa kina juu ya ushahidi ulioletwa mbele yake asipofanya hivyo hiyo hukumu inakuwa ni batili.
"Kila hakimu au jaji anayo staili au utaratibu wake wa kuandika hukumu lakini kitu cha msingi anachotakiwa kuangalia ni kupitia viini vyote vya mashitaka na ushahidi kama ulivyotolewa na pande zote," ameeleza Magafu huku akirejea mashauri yaliyowahi kufanyiwa uamuzi na mahakama ya rufani na kuongeza.
....Mheshimiwa Jaji, hakimu aliyesikiliza hili shauri hakufanya uchambuzi wa kina matokeo yake akatoa hukumu ambayo tunaiona haikuwa stahiki. Kama mheshimiwa hakimu angefanya uchambuzi wa kina juu ushahidi ulioletwa mbele yake angeweza kugundua mambo yafuatayo.
....Hati ya mashitaka iliyoletwa mbele yake haikukidhi matakwa ya kisheria ilikuwa 'defective' Ushahidi uliotolewa haukuendana na mashitaka yaliyokuwa mbele yake,".
Magafu alidai kuwa kesi iliyofunguliwa na kuwafunga wateja wao ilikuwa ya majungu na ilisababishwa na polisi kutofanya upelelezi ipaswavyo.
"Kwa nini polisi wanatakiwa kufanya upelelezi na upelelezi uwe wa kina ili waweze kugundua kosa limefanyika au halikufanyika kama kesi ni ya majungu au si majungu katika hii kesi tunayoona hapa ilikuwa ya majungu," amedai wakili Magafu na kuongeza
...Pw 6 ( shahidi wa sita wa Jamhuri, Bakari Msangi) na mleta rufaa wa kwanza , (Sabaya) walikuwa wanatofautiana walipokuwa UV CCM na PW 6 hakufurahi mleta rufaa wa kwanza kuteuliwa kuwa DC hakufurahi.
....Polisi wangechunguza vizuri wangejua ni uongo. Pw 6 anasema alipekuliwa akaibiwa 390,000 na simu lakini pw 4 anasema alishuhudia PW 6 akipekuliwa alichoshuhudia aliona akinyang'anywa simu na wallet," .
"Kwenye ukurasa wa 113 ya uamuzi mahakama ilieleza kwenye hoja za majumuisho za mawakili . Mahakama ilisema kuwa shahidi wa saba na wa 11 wote wawili walisema duka hilo liko Bondeni Street karibu na Soko Kuu tunajiuliza hilo ni sawa?
...Kwenye ukurasa wa 124 Gwakisa anasema kuwa alifahamishwa na mrufani wa kwanza bw. Lengai ole Sabaya kuwa aliwakamata PW2 ( Noman Jasin) na PW 4 (Hajirini Saad) kwenye duka lao huo sokoni.
...Siku ya tarehe 12 /1 / 2021 (Gwakisa) alienda yeye PW 7 PW 2, PW4 kwenye duka la PW 2 na PW 4 lililoko bondeni street lililoko karibu na Soko Kuu. Duka linalozungumziwa hapa ni la pw 1 (Mohamed Saad lililopo bondeni street near market . Pw 7 hakuwahi kuzungumzia duka la PW 1 ambalo ndilo lipo kwenye hati ya mashitaka,"..
"Mheshimiwa Jaji issue sio kumiliki duka ila ni kumiliki duka eneo ambalo tukio wa unyang'anyi wa kutumia silaha umefanyika. Pw 1 (Mohamed Saad) anaonekana kuwa na maduka zaidi ya matatu. Duka la kwanza liko bondeni street ambalo haliungwi mkono na ushahidi wowote," amedai wakili Mahuna na kuongeza.
...Duka la pili ni hili lililopo mtaa wa sokoni ambalo hata yeye anasema , duka la tatu lipo Bondeni Kati kulingana na PW 7 (Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha, Gwakisa Minga)na duka la nne ni la TIN linasema Shaahid Store linaonekana liko Nyamwezi.
.,Ni duka lipi linaloungwa mkono na hati ya mashitaka ni lipi?Kuna makosa kusema ushahidi wa mashahidi wa saba na wa kwanza wanashabihiana kwenye eneo kwani wametofautiana kama nilivyoeleza hapo juu,"
Waleta rufaa wengine kwenye shauri hilo linalotokana na kesi ya jinai namba 129/2021 ni Silvester Nyengu, Daniel Mbura wanaowakilishwa na mawakili Edmund Ngemela
Silvester kahunduka na Fridolini Bwemelo.
Ambapo Mleta rufaa wa kwanza, Sabaya mbali na mawakili Magafu, Mahuna pia anatetewa na wakili, Faudhia Mustafa.
Upande wa Jamhuri umewakilishwa na mawakili waandamizi, Ofmed Mtenga, Veriana Mlenza na wakiki wa Serikali, Baraka Mgaya
0 Comments:
Post a Comment