“Suala la idadi ya watu ni kubwa. Kumbe huko nyuma kulishakuwa na mapendekezo. Yeyote anayeona anaweza kuishi mahali pengine yuko huru kusema. Kama yuko mtu wa aina hiyo, awe huru kwenda kwa DC (Mkuu wa Wilaya) kajiandikishe na Serikali itakuhudumia vizuri," amesema Mjaliwa na kuongeza.
....Hayo ni maamuzi ya mtu binafsi, kusiwe na mtu wa kumshinikiza fulani asifanye maamuzi yake. Kama yuko aachwe afanye maamuzi yake, aseme anataka kwenda wapi na sisi tutamhudumia.”
Majaliwa alitoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 17, 2022) wakati akizungumza na viongozi na wananchi wa tarafa ya Ngorongoro kwenye kikao cha ndani kilichofanyika makao makuu ya zamani ya NCAA, wilayani Ngorongoro.
0 Comments:
Post a Comment