MAJALIWA: WANANCHI, WAHIFADHI WAJUI MIPAKA YA USHOROBA WANAOGOMBEA




 Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa amesema katika suala la ushoroba wa kilometa za mraba 1,500 lililopo Loliondo kumekuwa na ubishi wa muda mrefu juu ya eneo tajwa lakini hakuna anayejua mipaka halisi ya eneo hilo.

 

“Ubishi ubishi wa eneo kwenye namba upo kati ya wenyeji na wahifadhi lakini hakuna anayejua kiuhalisia eneo linaanzia wapi na linaishia wapi. Haya ni maamuzi ya mwaka 2018 yaliyofikiwa kwenye kikao cha Ololosokwan," amesema Majaluwa na kuongeza.

...Ni vema tukaweka alama za kudumu ili iwe rahisi kubaini eneo hilo; kilometa za mraba 1,500 zijulikane zina ukubwa gani na zinagusa eneo lipi,”.

 

“Hakuna jambo linataka kufanywa kwa trick kwa kutaka kumuathiri Mtanzania, hakuna Serikali ya namna hiyo. Kila jambo linalozungumzwa kwenu ni jema tu, linafanywa kwa nia njema.”

0 Comments:

Post a Comment