Tanzania yashiriki Maonesho ya Utalii Hispania




Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki Maonesho ya Utalii nchini Hispania yanayofahamika kama FITUR kuanzia Januari 19 hadi 23, 2022.



Maonesho ya Fitur yanayofanyika katika Jiji la Madrid ni mojawapo ya maonesho makubwa ya utalii duniani na Hispania ni  nchi ya 11 kwa kuleta  watalii wengi nchini Tanzania.


Maonesho haya yanafanyika kwa mara ya kwanza kwa kukutanisha nchi mbalimbali baada ya kutofanyika mwaka jana 2021 kutokana na janga la UVIKO 19

0 Comments:

Post a Comment