SABAYA ALIA NA WAFANYABIASHARA KILIMANJARO

 



 

ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amedai kuwa Rais alimsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi lakini hakupewa haki ya kusikilizwa badala yake akafunguliwa mashitaka ya uongo mahakamani .

 

Aidha ameendelea kuhusisha kesi inayomkabili na siasa za wilaya ya Hai huku akidai kuwa kiongozi wa kitaifa wa chama cha upinzani alitumia wafanyabiashara wenye ushawishi ili apate matatizo jambo alilodai kuwa wamefanikiwa.

 

Aliyasema hayo jana wakati akiuloizwa maswali ya dodoso na wakili wa utetezi, Syvester Kahunduka mbele ya hakimu Mkazi, Patricia Kisinda wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha anayesikiliza shauri hilo la uhujumu Uchumi namba 27/2022.


Sabaya ambaye anajitetea yeye akiwa ni shahidi wa pili alidai kuwa bada ya kusimamishwa ukuu wa wilaya na Rais hakuwahi kupewa nafasi ya kusikilizwa badala yake alifunguliwa kesi za uongo.

 

Sehemu ya maswali ya dodoso aliyoulizwa Sabaya na  wakili wa utetezi, Sylvester Kahunduka

Wakili:Ile namba ulisajaili kwa ajili ya biashara za familia wewe ulikuwa unatumia namba gani?

Shahidi:Hadi tarehe 27.5 nilikuwa natumia namba mbili 0714 028888 na 0754 585458

 

Wakili:Inasemekana ulipokea shilingi milioni 90 kuna mtu yeyote aliyeliona na kuja kuthibitisha hilo

Shahidi:Hakuna mtu yoyote aliyekuja akasema amenikabidhi au ameshuhudia nikikabidhiwa milioni 90

Wakili:Unamjua vipi Philip Haule Njombe?

Shahidi:Simjui

Wakili:Si kweli kwamba hawajasema sasa mtu huyo yuko wapi?

Shahidi:Hawajawahi

Wakili:shahidi kuna wakati ulikuwa unalalamika shahidi wa 13 ( Afisa Uchunguzi kutoka TAKUKURU Ramadhan Rajab Juma) anashirikiana na watu kukuangamiza uonekane una ‘image’ mbaya kwa jamii ulikiwa unamaanisha kitu gani.

 

Shahidi:Mimi nilikuwa Dc Hai, Kilimanjaro na huko Hai,ni jimbo la uchanguzi ambapo kulikuwa na mbunge ambaye aliamini hawezi kuacha ubunge maisha yake yote. Mbunge huyo ambaye ni mwenyekiti  wa upinzani Taifa alitumia ushawishi wake akidhani mimi ndiyo nazuia ubunge wake 2020 nikiwa nahudumu kama DC alitumia ushawishi wake wote kuhakikisha ananidhibiti ili apate ubunge wake.Na aliwatumia wafanyabiahsara wenye ushawishi ili niingie kwenye matatizo na amefanikiwa

 

Mh. hakimu kuwa mbele yako leo nikiwa hai nashukuru kwani mipango iliyokuwepo ni ya kuondoa kabisa uhai wangu.Mimi ni sehemu ya siasa hizo sikutegemea shahidi wa 13 asingeingia kwenye mtego wa kufanya siasa katika mazingira ambayo mimi tu nilipewa haki ya kusikilizwa na nilinyimwa kwa makusudi.


Wakili:Alichoeleza Rais sicho kilichofanyika ulikwa unamaanisha kiti gani?

Shahidi:Mh hakimu Rais alitoa maelekezo ya kunisimamisha ili kupisha uchunguzi na ilikuwa busara unachunguza jambo ambalo huna uhakika nalo ndo maana nilipaswa kupewa haki ya kusikilizwa.

 

Sikuwahi kupewa hiyo haki zikatengenezwa kesi za uongo. Naona ile haki niliyopewa nilinyang’anywa na watu waliotumia kwa maslahi yao



Baada ya mawakili wa utetezi ambao wanwatetea washitakiwa wenghine kumaliza kumuuliza Sabaya maswali ya dodoso upande wa Jmahuri waliomba shauri hilo liahirishwe kwani muda uliokuwa umebaki ni mdogo .


Hakimu Kisinda aliahirisha shauri hilo mpaka Februari 2, mwaka huu litakapokuja kwa ajili ya upande wa Jamhuri kumuuliza maswali ya dodoso.


"Wiki inayokuja hatutaweza kuendelea na kesi kwa sababu ni wiki ya sheria hivyo tutaendelea tarehe mbili mwezi wa pili," alisema Hakimu Kisinda akiahirisha shauri hilo.



0 Comments:

Post a Comment