Aidha amedai kesi ya
uhujumu uchumi iliyopo mahakamani
inatokana na maumivu ya wafanyabiashara wa Kilimanjaro kutokana na mtu wao
kukosa ubunge.(hakumtaja jina)
Pia amemtaka shahidi wa 13 upande wa Jamhuri, Ramadhani Rajab
Juma, (39) aache kutengeneza magenge kwa madai kuwa anakutafuta watu waseme
walimpa hela kwa kile alichoeleza kuwa hiyo si kazi ya serikali.
Sabaya ameyasema leo,
Januari 19,2022 wakati akiongozwa na wakili wake, Moses Mahuna kutoa ushahidi
wake mbele ya Hakimu Mkazi, Patrisha Kisinda wa mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha.
Sabaya ambaye
anajitete kama shahidi wa pili amedai kuwa Ramadhani ambaye ni afisa uchunguzi
wa TAKUKURU analipwa na wafanyabiashara wa mkoani Kilimanjaro ambao hakuwataja.
“Maumivu ya
wafanyabiashara wa Kilimanjaro kwa ajili ya mtu wao kushindwa wasiniwekee mimi
kwa sababu ni chombo cha dola,” ameeleza Sabaya na kuongeza.
…Niliweka uhai wangu
rehani nikifanya kazi za serikali mpaka nikatumiwa watu wa kuniua sasa Ramadhani
kama chombo cha dola anatakiwa akae upande wa serikali sio kutengeneza magenge
na kutafuta watu waseme tulimpa Sabaya pesa hiyo si kazi ya serikali”.
Kisha Wakili wake,
Mahuna akamuuliza shahidi wa 13 alisema shahidi huyo wa 13 alisema alipata taarifa
fiche akasema uligawa fedha kwa vijana wako pale Tulia ... tena anadai mlikuwa
chumbani.
Sabaya akakaa kwenye
kiti kisha akawa anatokwa na machozi jambo lililomfanya wakili wake kusema “
Mheshimiwa naomba shahidi apumzike kwa sababu kuna mambo yanamfanya apate hisia.
Mheshimiwa naomba nitoe swali hilo nitauliza lingine manake linampelekea shahidi
kujisikia vibaya,”.
Maswali na majibu
Sabaya akiongozwa na wakili wake, Moses Mahuna kutoa Ushahidi
Wakili:Lengai hapa
mahakamani alikuja shahidi wa jamhuri namba 13,akasema wakati wa upelelezi wake
alienda Kilimnajaro na alipofanya mahojiano na baadhi ya watu akiwemo shahidi
wa kwanza aliambiwa wewe hukuwa na mahusiano mazuri na Mkuu wako wa mkoa wewe hulo
unalizungumziaje?
Shahidi:Mheshimiwa Hakimu huyo shahidi namba moja aliyemweleza
shahidi namba 13 hayo,hakuna popote shahidi huyo wa kwanza alipodai mimi nilikiwa DC Hai sikuwa na mahusiano
mazuri na aliyekiwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Alichokiwa anafanya shahidi
wa 13 aliacha upelelezi akaenda kuokota aina ya siasa zilizokiwa Kilimanajro
akaleta hapa mahakamani.
Ni shahidi muongo
aliyeacha upelelezi akajiingiaza kwenye siasa akaacha taaluma yake
Wakili:Pia hapa
mahakamani alikuja shahidi 10 Francis Mrosso,alisema anakufahamu kwa
kukuona kwenye Tv au social media lakini alidai kwamba kabla ya siku ya 22/1/2021
aliwahi kukuona wewe kwenye mazishi katika wilaya ya Hai na yeye alienda mwenge
mazishi hayo sababu rafiki yake anayeitwa Tosh alifiwa na mtoto.Wewe una utetezi
gani juu ya madai hayo ya bwana mrosso.
Shahidi:Simfahamu mtu
anayeitwa Tosh wala siwezi kwenda kwenye mazishi ya mtoto nisiyemfahamu.Taarifa
hizo kama zilikuwa za kweli angeeleza katika maelezo ya polisi
Huo ushahidi alioutoa
ni wa uongo.
Wakili:kwanini unasema
hujahusika na mkataba huu wakati kuna sahihi yako kwenye mkataba huu?
Shahidi:Mheshimiwa
Hakimu huu mkataba siutambui na mawakili wangu walieleeza hivyo na kwa kuwa
nilishakanusha ilikuwa kazi ya mashtaka kuthibitisha huu mwandiko na hii sahihi
ni ya kwangu.Hawakukiunganisha kwa sababu walijua italeta matokeo wasiyoyapenda.Hii
sahihi siyo ya kwangu.
Wakili:Shahidi hapa
mahakamani alikuja shahidi tatu, Adanbest Marandu,anasema yeye ni mlinzi wa
getini na tarehe 22/1/2021 aliingiza rekodi za magari na moja T 144 CZU,STL
5434 na T 846 CTU alisema alikuona wewe ukiingia na magari hayo. Wewe kwa
ushahidi huo una utetezi gani?
Shahidi:Kati ya hizi
gari tatu sifahamu gari lolote.
Mkanganyiko kwenye maelezo ya mtu aliyeleta kielelezo hiki na alieleza mahakama
kuwa haoni kwa miaka sita iliyopita. Hangeweza kuandaa kulelezo hiki na aliaema
alisaidiwa kuandika magari haya na Mrosso .
Wakili:Kililetwa kilelezo cha pili ni hati ya kuomba kupatiwa taarifa, ndiyo kilipelekea kupatikamaa kielezo cha tatu cha utetezi wako ukoje kuhusiana na kielelezo cha pili.,
Shahidi:Hii barua inatoka Takukuru kwenda kwa Mkurugenzi mkuu wa Vodacom pamoja na maekezo mengine barua imeomba mawasiliano ya simu na sms katika kipindi cha 20/1/2021 hadi 25/1/2021 zimeombwa namba tatu 0758 707171 Lengai ole Sabaya 0759 78686 Enock Mnkeni 0746 935569 Ramwel Macha.
Naombaa mahakama inipe kielelezo namba tatu,
Barua inayotoka vodacom
kwenda PCCB kwenye maelezo wanasema pamoja na barua hii 0746 935569
haijafanya mawasiliano katika kipindi hiki……
Shahidi 10 na 13 wakadai ndani ya ile gari alimtambua kijana mmoja mshitakiwa wa sita akisema alitumia simu yake kufanya mawasiliano na mshitakiwa wa kwanza
Wakili:Sasa bwana
Lengai hapa mahakamani alikuja shahidi wa 13 anasema katika upelelezi wake alibaini kwamba
wewe Sabaya na watu aliowaita vijana wako mliunda genge na mlikutana Point Zone
(hotel) kupanga kwenda Kwa Mrosso ili kutenda makosa ya kihalifu wewe una
utetezi gani juu ya amdai haya
Shahidi: Hilo ni genge
la Ramadhani analipwa wafanyabishara ….
Maumivu ya
wafanyabiashara wa Kilimanjaro kwa ajili ya mtu wao kushindwa ubunge wasiniwekee
mimi kwa sababu ni chombo cha dola ….Niliweka uhai wangu rehani nikifanya
kazi za serikali mpaka nikatumiwa watu wa kuniua sasa Ramadhani kama chombo cha
dola anatakiwa akae upande wa serikali sio kutengeneza magenge na kutafuta watu
waseme tulimpa sabaya pesa hiyo si kazi ya serikali.
Wakili: Shahidi huyo
wa 13 alisema alipata taarifa fiche akasema uligawa fedha kwa vijana wako pale
Tulia hoteli ... tena anadai mlikuwa chumbani.
Shahidi: Kimya akakaa
kwenye kiti akawa anatokwa na machozi.
Wakili:Mheshimiwa naomba shahidi apumzike kwa sababu kuna mambo yanamfanya apate ‘feelings’ (hisia).
Mheshimiwa naomba nitoe swali
hilo nitauliza lingine manake linampelekea shahidi kujisikia vibaya....Huku
Sabaya akilia wakili wake akachukua chupa ya maji kutoka kwenye meza ya
mawakili wa Serikali akayakataa akasema amefunga.
AKAENDELEA
KUHOJIWA
Wakili:Hapa mahakamani
unashtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2021 wewe na watu wengine sita jumla mnakua
saba unamfahamuje mtu anaitwa Enock Chagulani
Shahidi:Simfahamu mheshimiwa
hakimu hadi tarehe 4/6 tulipopandishwa
naye mahakamani kwa mara ya kwanza.
Wakili:na je
unamfahamuje mshitakiwa Watson
Mwahomange
Shahidi:Sijawahi
kumsikia simfahamu nilisikia jina hilo wakati linasomwa mahakama tarehe 4/6.
Wakili:Na je
unafahamije mshitakiwa wa nne John
Aweyo?
Shahidi:Simfahamu naye
nimfahamu siku hiyo tarehe 4/6.
Wakili:na je
unamfahamuje mshitakiwa wa tano Silvester Nyegu
Shahidi:Nilikuwa
namuona kama watumishi wengine anaofanya kazi chini ya ofisi ya DED (MKurugenzi Halmshauri ya wilaya) Hai,alikuwa miongoni mwa hao watumishi
Wakili:na kuana mtu
anaitwa Jackson Macha je unamfahamuje
Shahidi:Mheshimiwa
huyo tarehe 21.6.2021 aliletwa gerezani akiwa na mshitakiwa wa saba na walipifika gerezani niliambiwa wananitafuta
wakaniuliza mimi ndiyo Sabaya wakasema wameunganishwa kwenye kesi yangu
waliponitafuta ndio
niliwaona kwa mara ya kwanza
Wakili:unaposema gerezani
unamaanisha nini.
Shahidi:Gereza Kuu Kisongo
Wakili:Sasa kuna mshtakiwa wa mwisho Nathan Msuya huyu yeye naye
unamfahamu vipi?
Shahidi:Huyo mshitakiwa
wa saba alikuja na mshitakiwa wa sita gerezani
wakiulizia Sabaya ni nani na wakaniambia wameunganishwa kwenye kesi
inayonikabili na hawakuwa wananifahamu.
0 Comments:
Post a Comment