Na Gift Mongi, Moshi
Mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro Dkt Charles Kimei amesema deni la taifa bado ni stahimilivu na kuwa si tishio kama ambavyo
inasemekana ambapo pia nchi nyingi duniani zimekuwa zikikopa ili
kujenga miundimbinu ambayo itawawezesha wananchi wake kufanya biashara sambamba na huduma mbali mbali.
Dkt Kimei alitoa kauli hiyo katika hafla ya kupokea vyumba 85 vya
madarasa vilivyojengwa kwa shilioni bilioni 1.7 fedha ambazo ni kwa
maendeleo ya ustawi wa taifa katika mapambano ya ugonjwa uviko 19
ambapo zoezi hilo kwa wilaya ya Moshi lilifanyika katika shule ya
sekondari Himo kwa kukabidhi vyumba vinne.
Kwa mujibu wa mbunge huyo ambaye pia ni mtaalamu wa uchumi na amewahi
pia kuhudumu katika sekta kadhaa za fedha nchini ikiwemo mkurugenzi
mtendaji wa benki ya CRDB ni kuwa bado taifa letu lina sifa za
kukopesheka na ndio maana tumeendelea kuaminiwa na wahisani
mbalimbali ikiwemo mfuko wa fedha duniani na benki ya dunia.
“Sisi bado tupo katika hali nzuri ya kukopesheka na ndio maana rais
Samia Suluhu Hassan alivyoenda kukopa aliaminiwa mra moja tofauti
labda na mataifa mengine sisi bado tunayo rekodi nzuri katika mkopo na
suala la mkopo si aibu hatuanza sisi kukopa wala hatutakuwa wa
mwisho”alisema
0 Comments:
Post a Comment