CCM KUHAKIKISHA VIJANA WANAWAKE NA WALEMAVU WANAKOPESHWA

 Na Gift Mongi,Moshi

CHAMA  Cha mapinduzi, (CCM) kitaendelea kusimamia ilani yake katika kuwawezesha vijana wanawake na wenye ulemavu kuwapatia mkopo usiokuwa na riba kutoka katika vyanzo vya ndani vya halmashauri lengo likiwa ni kuwakwamua kiuchumi.


Hali kadhalika serikali ya CCM itaendelea kuunga mkono vikundi mbalimbali vya vyama vya kuweka na kukopa kwa lengo la kurahisisha huduma za kifedha karibu zaidi na jamii.



Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi aliyasema hayo Mara baada kukabidhi msada  vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa Chama Cha  ushirika wa akiba na mikopo Cha Umoja saccos kilichopo kata ya Kimochi wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.


"Dira na dhamira ya chama Cha mapinduzi ni kuhakikisha wale wajasiriamali wasio na mitaji wanaipata kupitia taasisi zisizo na masharti magumu ikiwemo hii saccos na ndio maana nimehamua kuja kuwaunga mkono"alisema


Alisema kukamilika kwa ofisi hiyo kutaenda kuongeza wigo mpana katika kuhidumia jamii hususan kwa wale ambao hawajaweza kukidhi viwango vya kupata mikopo kwenye taasisi kubwa ikiwemo benki.


Kwa upande wake meneja wa chama hicho Kulwa Mgeni mbali na kumshukuru mbunge huyo kwa msaada wa vifaa hivyo amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutaenda kuongeza ufanisi nanwigo mpana katika kuwahudumia  wananchi.


" Kumalizika kwa ujenzi wa jengo hilo kutarahisisha huduma za kibenki pamoja na zile za chama kwa wanachama na wananchi wa eneo hilo tofauti na sasa na kuwa lengo ni kuwafikia wananchi wengi zaidi"alisema


Naye diwani wa Kata hiyo ya Kimochi Ally Badi alisema ni hatua muhimu inayopaswa kuungwa mkono na wadau wa maendeleo ili kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi.

0 Comments:

Post a Comment