MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA MONABAN NA BARAKA WALIVYORUSHA RISASI HADHARANI


MFANYABIASHARA maarufu jiji Arusha, Philemon Mollel, maarufu kama Monaban,(63), na mwenzake Baraka Taitas Mollel, (43) wamesomewa maelezo ya awali kwenye kesi ya matumizi mabaya ya Silaha inayowakabili.

Aidha upande wa jamhuri unatarajia kuleta mashahidi sita na vielelezo 16 mahakamani hapo.


Wamesomewa maelezo hayo leo Septemba 7, 2021 na wakili wa serikali, 
Blandina Msawa mbele ya hakimu Mkazi,Salome Mshasha,wa mahakama hakimu Mkazi Arusha, anayesikiliza shauri hilo la jinai namba  80/2021.



Aliieleza  mahakamani huyo kuwa mnamo Mei, 18 mwaka huu Mshtakiwa wa kwanza,
 Philemon katika eneo la kituo Cha mafuta Cha Saiteru kilichopo Ngulelo wilaya ya Arumeru,alifyatua risasi kwa kumwelekezea mshtakiwa wa pili (Baraka) ambaye naye alijibu mapigo Kwa kufyatua risasi hewani.

Alisema tukio hilo lilisababisha taharuki na hofu Kwa Jamii na wakazi wa eneo hilo,ambapo ni kinyume Cha kifungu namba 84 na 35 Cha sheria ya kanuni ya adhabu ya mwaka 2019.

Alieleza kuwa washtakiwa hao walikamatwa eneo la tukio na kupekuliwa katika maungo Yao na nyumbani kwao na kupatikana na silaha aina ya bastola na risasi.

Wakili wa serikali Msawa aliendelea kueleza kuwa kuwa mshtakiwa wa kwanza Philemon,  alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na bastola moja yenye risasi 25 ,Magazini mbili na leseni ya silaha hiyo.

Aliendelea kueleza kuwa  mshtakiwa namba mbili Baraka alipopekuliwa  alikutwa na bastola moja na leseni ya silaha hiyo.

Washtakiwa wote  walikana mashitaka hayo ambapo shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa Septemba 27 mwaka huu.

Mshitakiwa wa kwanza, Philemon anatetewa na wakili Kapimpiti Mgalula huku mshitakiwa wa pili, Baraka akitetewa na wakili, David Makata.

0 Comments:

Post a Comment