WATU watano wafariki na mmoja kujeruhiwa baada magari mawili aina ya Mitsubish Fuso na lingine Mitsubish Canter kugongana uso kwa uso eneo kwenye barabara ya Arusha/Moshi eneo la konoike kijiji cha Kolila Tarafa ya king’ori wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, (RPC), Justine Masejo imeeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ilitokea leo majira ya zaa 10:00 Alfajiri ni mwendoka kasi.
Ameeleza kuwa gari lenye namba za usajili T 111 CUU aina ya Mitsubish Fuso lililokuwa linaendeshwa na Heriel Lyimo, (42) mkazi wa Holili, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T.612 BNN aina ya Mitsubish Canter iliyokuwa ikiendeshwa na Peter Mmasi ambaye bado umri wake na makazi yake hayajafahamika.
RPC, Masejo, amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni dereva wa gari aina ya Mitsubishi Canter, Peter Mmasi, Victor Kileo, Vivian Urio na Isack Temba ambao walikuwa abiria wa gari aina Mitsubish Canter na ni wakazi wa Baraa jijini Arusha.
Amesema kwenye gari aina ya Mitsubish Fuso aliyefariki ni utingo wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Idd mkazi wa Himo mkoani Kilimanjaro ambapo Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Jijini Arusha.
Taarifa yake imeeleza kuwa majeruhi katika ajali hiyo, Heriel Lyimo ambaye amepelekwa katika hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro kwa matibabu zaidi.
Kamanda Masejo amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari aina ya Mitsubishi Fuso iliyokuwa inatokea Moshi kuelekea Arusha ambapo ilihamia upande wa pili wa Barabara na kugongana na gari aina ya Mitsubish Canter lililokuwa linatokea Arusha kuelekea Moshi.
Kwenye taarifa hiyo RPC huyo amesema kuwa baada ya magari hayo kugongana, gari aina Mitsubish Fuso lilipitiliza na kuanguka kwenye mtaro uliopo pembezoni mwa barabara.

0 Comments:
Post a Comment