MAHAKAMA ya Hakimu
Arusha, limetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na mawakili wa utetezi
kwenye kesi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake
sita waliyokuwa wakipinga mahakama kupokea Counter book linalodaiwa kuorosha magari yalikuwa kwenye msafara wa Sabaya..
Uamuzi huo mdogo
umetolewa leo Septemba 30, 2021 na Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda anayesikiliza
shauri hilo la uhujumu uchumi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na
kuahirisha shauri hilo kwa muda kwa ajili ya kutoa uamuzi.
Amesema kuwa, mahakama
imefikia uamuazi huo kwa kuangalia
ushahidi uliotolewa na shahidi wa tatu wa jamhuri, Adanbest Marandu,(61) ambaye
ameieleza mahaka hiyo kuwa ana uelewa wa kutosha juu ya kielelezo alichotaka
kukiwasilisha mahakamani hapo.
“Pingamizi kuwa
kielelezo hakijafuata matakwa ya kisheria na shahidi kihalali hana
uhalali wa kutoa kielelezo hicho mahakamani, mahakama imetupilia mbali na kukubali kielelezo hicho,”
amesema Hakimu Kisinda wakati akitoa uamuzi huo mdogo.
Shahidi wa tatu upande wa
Jamhuri, Adanbest Peter Marandu, (61) ambaye ni muangalizi wa geti (mlinzi)
mfanyakazi kwa Fransis Mrosso akiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi,
Tarsila Gervas kutoa ushahidi wake
Sehemu ya mahojiano hayo
yalikuwa kama ifuatavyo;
Wakili: Mzee Marandu
unaishi wapi?
Shahidi: Shamsi
Wakili: Shamsi iko wapi?
Shahidi: Kata ya Elerai
Wakili:Una elimu gani?
Shahidi:Darasa la saba
1968-1975
Wakili:Unafanya kazi
gani Arusha?
Shahidi:Nafanya kazi kwa
Francis Mrosso,mwangalizi wa geti
Wakili:Huyu Mrosso hilo
geti unangaalia linahusu nini?
Shahidi:Magari ya
kufanyiwa service na pump
Wakili:Hii kazi ya
uangalizi kwa Mrosso umeifanya kwa muda gani?
Shahidi: Miaka sita
Wakili: Wewe
kama.mwangalizi wa geti ni majukumu yapi unayo?
Shahidi: Kufugulia
magari yanayoingia na kutoka, kuandika magari ‘time’ (muda) ya kuingia na
kutoka na limeenda kwa nani
Wakili: Kitu kingine
unachifanya?
Shahidi:Kutunza counter
book yangu
Wakili:Hili ‘counter
book’ linahusiana na nini?
Shahidi:Kurekodi magari
yaliyoingia
Wakili:Hili ‘Counter
book’ unalitunzia wapi/
Shahidi:Nalitunzia pale
pale ‘yard’.
Wakili:Hii yard iko wapi?
Shahidi:Iko Mbauda
Wakili:Hilo ‘counter
book’ unaweza kulielzea likoje?
Shahidi:Ni jeusi, lina
karatasi nyeupe juu na imeshikiliwa na solo tape,
Wakili: Mwonekano
wake?
Shahidi:Kwa ndani
ukifungua nimeandika namba za simu za watu waliongia ndani nyuma ya hiyo
counter book,nimechora mistari minne ya kutenganisha
Wakili:Umeeleza hili
kaunta ndiyo unaweka rekidi za magari unaziwekaje?
Shahidi:Naandika tarehe
na mwezi na code namba halafu gari linapoingia naandika namba zake na linaenda
kwa nani na muda wa kuingia na kutoka
Wakili:Umesema unaingiza
code namba ni utambulisho wa nini?
Shahidi:Code namba ya
utambulisho kati ganvy na mwenzangu ay boss wangu
Wakili:Hii code inatokana
na nini?
Shahidi:inatokana na
tarehe
Wakili:umeeleza
unaandika gari linaenda kwa nani kwa nini?
Shahidi:Nimeelekezwa na
bosi ili ikitokea gari la mtu limetokea tatizo ukicheki kwenye kitabu inaonyesha gari imeenda
kwa fulani
Wakili:Mzee Marandu
ukifika kazini asubuhi unafanya nini kuhusiana na counter book lako?
Shahidi:Nafanyia maaandalizi
kulingana na tarehe
Wakili:Umeeleza gari
inakoenda kwa namna inavyopaki mnapaki vitu?
Shahidi:Kila mtu na
kitengo chake hivyo inatokana na namna….
Wakili: Mzee Marandu tarehe
22/1/2021 ukisikia unapata kumbukumbu zipi
Shahidi: 22 januari
nakumbuka ilikuwa siku ya ijumaa,katika kumbukumbu yangu nilifanya maandalizi pale getini
nikachukua kaunta nikajaza tarehe,code namba 1730. Nikapokea magari hadi saa
8:35 mchana kuna gari ziliingia 3 zikifatana niliandika kwenye kitabu
gari ya kwanza
Nakumbuka ulikuwa ni T 144 CZU, la pili likaingia STL 5434 na la tatu T 846 CTU.
Wakili: Unaweza
kukumbuka yalikuwa yanafananaje?
Shahidi:ile ya kwanza
ilikua rangi nyeusi ya pili nyeupe la tatu la tatu rangi ya ugoro
Wakili:Na baada ya
magari kuingia nini kiliendelea?
Shahidi:Niliona watu saba
walishuka wakaangaza macho kushoto kulia
kushoto kulia wakaingia kwa Mrosso wakatoka nje mmoja akabaki ndani. Sikujua
kilichoendelea mle ndani kwani getini hadi ofisini ni hatua 60
Wakili:Hao watu saba
ukiambiwa umzungumzie mmoja mmoja unaweza kuwazungumziaje?
Shahidi:Sitaweza
kuwazungumzia chochote.
Wakili: Umsema uliona
watu saba fafanua uliona nini?
Shahidi:Walishuka
wakaingia ndani mmoja akabaki wengine wakabaki ..Nilimuona akiwa ndani kwa
mhasibu.Huyo bwana niliyemuona pale ni mtu mmoja anaongea na mhasibu,nilimuona
Sabaya.
Wakili:Sabaya ni nani
Shahidi:Mkuu wa wilaya ya
Hai
Wakili:ulifahamuje ni
Sabaya na ni DC wa Hai?
Shahidi:Huwa namuona
kwenye TV
Wakili:Na kwa kuwa
ulimuona na namna ulivyomfahamu kwa hiyo siku alikuwa yukoje?
Shahidi:Alikuwa amenyoa
panki,amevaa kaunda suti ya mikono mirefu ya rangi kama bluu alikuwa amenyoa oo
Wakili:Sasa mzee Marandu
hii siku uliandika kwenye counter book, nikikuonyesha hilo counter boook utawezaje kuthibitisha hiki ndo kitabu
ulichoandika magari uliyoyataja?
Shahidi:Lina rangi
nyeusi,ina karatasi nyeupe juu imeshikiliwa na solo tape
Tar 22 code namba 1730
Kingine tarehe 23/1/2021
boss alinifuata akaniuliza kama nimeandika zote nikamtajia namba zake tofauti
na magari mengine yote.
Wakili: Mzee Marandu
baada ya kumtaja Sabaya kumuona nini kiliendeela akiwa ofisini
Shahidi: Sikujua
chochote kilichoendelea ila walitoka tena kwa pamoja magari yote na Mrosso
alitoka nje ya geti kwa miguu akiwa na mtu mmoja kati ya wale. Magari yalitoka
saa 9:15
Wakili: Kuna daftari
naomba nimpe shahidi aweze kueleza hii mahakama ni nini?.
Liangalie tueleze ni
kitu gani?
Shahidi:hili ni counter book la kuhifadhi kumbukumbu yangiu
Wakili: Angalia maingizo
ya tarehe 22 angalia kama unaweza kutambua na ni kwa sababu zipi anayatambua?
Shahidi:Nimeyatambua
mimi ndo niliyerekodi magari yote
yaliyoingia code namba 1730 na maingizo ya magari matatu ambayo nimeweka tiki
haya hapa (huku akionyesha mahakama)
Wakili:Unaiambia nini mahakama
kuhusiana na maingizo hayo?
Shahidi:ningeiomba
mahakama ichukue kama kithibitisho.
Wakili wa utetezi, Moses
Mahuna akasimama: Utetezi mshitakiwa wa kwanza wa 1 na 2 tunapingamizi dogo la kisheria juu
ya kupokelewa kwa kitabu hiki. Mheshimiwa kabla ya kitabu kutolewa na tumekiona
kimetolewa kwenye mikoba ya wakili msomi wa serikali, Tarsila ndiye aliyekuja
na hiki kitabu kwenye mikoba yake. Wakili msomi hatuelewi hatuelezi yeye binafsi
alikipata wapi hiki kitabu ana anamuonyesha shahidi na kumtaka shahidi akitoe
mahakamani.
Kitabu chenyewe kinaonekana
kimetumika mwisho tarehe 27/5?2021 inaonyesha kilikuwa upande wa uchunguzi, wakili
hatuelezi chain of custody kama sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai
inavyoelekeza( akataja kifungu cha sheria).
Atueleze kimepatikanaje
wakili amekitoa wapi ni dhahiri kwamba ushahidi huu kwa namna yoyote vile kwa
kuwa hakuna na shahidi mwenyewe akatoa kwenye mifuko yake.
Ushahidi huu haukupatikana
kwa kufuata sheria umekiuka (anataja kifungu cha sheria na kufafanua )
Tunaomba ushahidi huu
usipokelewe ni batili umekiuka sheriia za nchi, sheria za makosa ya jinai.
Ni ombi letu mhakama
ikatae kupokea ushahidi huu
Wakili wa utetezi,
Freedoline Gwemelo: Tunapinga vikali kupokelewa kielelezo hiki tukisapoti yale
yote aliyosema wakili wa mshitakiwa wa kwanza na wa pili tukiongezea yafuatayo;
1.Msisitizo wa
sheria
Lengo ya kifungu ni
kuzuia ‘tamped’ ya kielelezo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine tuwe
na uhakika kielelzo hakijawahi kuwa na
hakijawa ‘tamped’.
Tunasisitiza kielelezo
hiki kisipokelewe kwa sababu kinatia shaka kwa sisi mawakili, watuhumiwa na
mahakama hii.
0 Comments:
Post a Comment