WAFANYABIASHARA jijini Arusha,waelezea kuridhishwa na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakidai imerejesha matumaini kwani imeweka mazingira mazuri kiuchumi sanjari na kuongeza mwingiliano wa kibiashara na mataifa mengine kuongezeka.
Aidha wamemuomba ashughulikie tatizo la ongezeko la mafuta ya petrol na dizel kwani inasababisha kupanda kwa gharama za bidhaa na huduma mbalimbali.
Waliyasema hayo kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki wakati wakitoa maoni juu ya wanavyoziona siku 100 tokea serikali hiyo iingie madarakani baada ya kifo cha mtangulizi wake, Rais wa awamu ya tano, Hayati, John Pombe Magufuli.
Mkurugenzi wa kiwanda Cha Magodoro Cha Tanfoam, Abbas Lalji alisema Rais, Samia amefanikiwa kupunguza changamoto za wafanyabiashara na kutengeneza mazingira rafiki ya kibiashara na ulipaji Kodi.
Alisema tangu aingie madarakani mwezi Machi mwaka huu amekuwa akikemea matumizi ya nguvu kwa Wafanyabiashara wakati wa kukusanya mapato ya Serikali na hivyo kuwaondolea hofu Wafanyabiashara ambao baadhi yao walilazimika kufunga biashara zao .
"Kwa Sasa tunachokiomba Serikali ipunguze kodi kwa malighafi zinazoingia nchini ili kuepusha kupanda kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na pia Kodi iwe moja na kuondoa utaratibu wa Sasa wa kila taasisi ya serikali kuchukua mapato ya Serikali "alisema Lalji.
Naye mkurugenzi wa kampuni ya Benson, Naushad Abbas na alisema kwa kifupi ambacho Rais, Samia aingie madarakani wafanyabiashara wamejawa na amani na anajisikia furaha kulipa kodi halaki kwa maendeleo ya Taifa.
"Tangia Mama Samia aingie madarakani Wafanyabiashara tumekuwa na hamu ya kuwekeza biashara zetu kila Mkoa na Mimi ningekuwa na uwezo mkubwa wa kifedha natamani kuwekeza kila Mkoa kutokana na mazingira mazuri ya biashara yaliyowekwa na mama yetu Samia kwa Sasa Sina (Stress) hofu tena,"alisema Naushad.
Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji ya Avco investment LTD ya jijini Arusha, Kakee Dhariwal, alisema tokea Rais Samia aingie madarakani mazingira ya biashara yameboreka sana na Serikali inawasikiliza Wafanyabiashara na kuwajengea mazingira mazuri.
"Katika kipindi Cha siku 100 biashara zimeongezeka sana hata ukienda katika mpaka wa Namanga utakuta magari zaidi ya 200 kila siku yakienda Kenya ama kuingia nchini. Hii ni wazi kwamba mazingira ya biashara ni mazuri," alisema Kakee.
Naye mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Dodoma Transport Agent LTD ,Sardul Singh Mand alisema uongozi wa Rais Samia umeleta mabadiliko makubwa hasa kwa Wafanyabiashara na wakulima ambapo ameweza kutatua kero zao.
"Mama Samia ameweza kuondoa dhana ya askari wa usalama barabarani kukusanya mapato kwa kuwapiga faini ovyo madereva wa malori Ila changamoto ya Sasa ni mafuta yamepanda Bei Sana tunaomba Rais Samia aliangalie hilo, "alisema
Mwakilishi wa kampuni ya Arusha Sundries tawi la Arusha, Sandeep Kumar alisema Rais Samia ameanza vizuri huku akiomba mazingira ya biashara yaendelee kuboreshwa ili uchumi wa nchi uendelee kukua kwa Kasi kubwa.
Mkurugenzi wa Cultural Heritage, Saifudin Khanbhai, aliipongeza Serikali kwa hatua ya kuruhusu maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kuendelea na shughuli zao kwa kuwarejeshea leseni zao walizokuwa wamezichukua akidai hatua hiyo itasaidia kukuza zaidi uchumi wa nchi na kufanya wananchi wawe na fedha za mfukoni ambazo zilipotea.


0 Comments:
Post a Comment