Na Gift Mongi, Moshi.
WAZIRI wa maji, Juma Awesso amemtaka mbunge wa jimbo la Vunjo Dkt. Charles Kimei kutokucheka na wataaalamu katika utekelezaji wa miradi ya maji katika jimbo la Vunjo kwani serikali katika bajeti iliyopita imetoa fedha za kutosha kuhakikisha wakazi wa jimbo la Vunjo wanapata maji safi na salama
Waziri wa maji Juma Aweso aliyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Njiapanda wakati wa ziara yake jimboni Vunjo mkoani Kilimanjaro kuangalia hali na mazingira ya vyanzo vya maji katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama
Alisema serikali inakwenda kujenga mradi wa maji katika kata ya Njiapanda wenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 kutoka katika chanzo cha maji cha Miwaleni na kuwezesha kuongezeka upatikanaji wa maji.
Alisema wakati serikali ikijipanga kuweza kuwaondolea wananchi tatizo la maji mamlaka za maji nchi nzima ziachane na tabia ya kuwabambikizia wananchi ankara za maji kwa kuwa sio lengo la serikali.
Maagizo hayo ya waziri Awesso aliyatoa Mara baada ya wananchi wa kata za Mwika Kusini na Njiapanda kulalamika kubambikiziwa ankara hivyo kutaka kuwepo na suala la uwazi wakati wa usomaji wa mita.
Alisema kumekuwepo na kasumba ya baadhi ya watumishi wa mamlaka hizo za maji nchini kusoma mita kwa wateja bila kuwashirikisha hali ambayo imekuwa ikileta malalamiko ya mara kwa mara jambo ambalo serikali kwa Sasa haitaweza.
Katika hatua nyingine waziri huyo aliwataka watendaji wa mamlaka za maji kuachana na visivyokuwa na tija vya mara kwa mara na badala yake wajikite katika kuhakikisha wanatatua changamoto za maji kwa wananchi kama ilivyo dira ya serikali ya awamu ya
sita.
Mbunge wa jimbo la Vunjo Charles Kimei alishukuru waziri huyo wa maji ambapo alisema fedha hizo zinatosha kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa jimbo hilo la Vunjo na kuahidi kulisimamia kikamili
"Tunamshukuru raisi Samia kwa kutupa kipaumbele sisi wakazi wa Vunjo na Hali ilivyo tunaenda kupata maji siku si nyingi na ndio uzuri wa kuwa na serikali sikivu inayoongozwa na chama cha mapinduzi"alisema
Katika ziara hiyo ya waziri wa maji katika jimbo la Vunjo miongoni mwa changamoto zililolalamikiwa na wananchi ni pamoja na changamoto ya upatikanaji wa maji na suala la wananchi kubambikiziwa ankara za maji na mamlaka ya maji safi usafi wa mazingira, (MUWSA).

0 Comments:
Post a Comment