POLISI WAMSHIKILIA MWANAJESHI KWA MAUAJI


JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, (JWTZ) (jina limehifadhiwa) wilayani Monduli kwa tuhuma ya mauaji ya mfugaji, Laisi Lemomo,  (26) mkazi wa kijiji cha Lashaine wilayani  Monduli Mkoa wa Arusha.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Justine Masejo ametoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Julai 13, mwaka huu akidai kuwa tukio  lilililotokea jana Julai 12, 2021 majira ya saa 10:00 Jioni huko katika kijiji cha Lashaine wilaya ya Monduli.

" Katika kubaini undani wa tukio hilo timu ya makachero imefika eneo la tukio na inaendelea uchunguzi wa tukio hilo na pindi Upelelezi utakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa,"amesisitiza RPC huyo.


Katika hatua nyingine jeshi hilo linamshikilia  kwa mahojiano mganga wa kienyeji  (jina limehifadhiwa) mkazi wa Sombetini jijini Arusha kwa tuhuma za kumshawishi mtuhumiwa wa tukio la ukatili dhidi ya Mtoto lililotokea Julai 06, 2021 maeneo la Burka.


RPC Masejo amesema mganga huyo wa kienyeji alikamatwa Julai 8, mwaka huu majira ya saa 07:00 mchana huko maeneo ya Sombetini katika Jiji la Arusha.

"Kama mnavyokumbuka tarehe 08 Julai mwaka huu tulitoa taarifa ya mtoto wa kiume mwenye miaka (4) ambaye alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia na kutekelezwa katika eneo la Burka," amesema kamanda Masejo na kuongeza.

"Katika uchunguzi wetu tumeweza kumhoji mganga huyo wa kienyeji mkazi wa sombetini ambaye amekiri kumshawishi mtuhumiwa huyo aliyemfanyia ukatili mtoto wa miaka minne (04) .

" Alimshawishi kwamba ukifanya kitendo hicho kitamsaidia katika kesi zake pamoja na utajiri katika biashara zake. Jeshi la Polisi linaendelea na Upelelezi pindi utakapokamilika Jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua za kisheria,".


Natoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za waganga wa kienyeji wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu ikiwa ni pamoja na kuwashawishi watu kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya kina mama na watoto,kwamba wakifanya hivyo watafanikiwa katika mambo yao mbalimbali.

IMETOLEWA NA: JUSTINE MASEJO-ACP KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA



0 Comments:

Post a Comment