![]() |
| ALIYEKUWA Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Saabaya leo Juni 18, mwaka huu akiingia kwenye mahakama ya hakimu Mkazi Arusha iliyopo maeneo ya Sekei |
Wananchi waliojitokeza nje ya mahakama wamesikika wakipaza sauti wakati Sabaya akishuka kwenye karandika la polisi na wengine wakimshangilia na wengine wakioaza sauti zaidi kumzomea huku wakiita 'mwizi' 'muuaji'.
Wananchi hao walianza kupiga kelele hizo baada ya mwananchi mmoja kumuona akishuka kwenye karandika na kumuita kwa sauti ambapo aligeuka na kupunga mkono ndipo wananchi hao walipoanza kupiga kelele za kushangilia huku wengi wakimzomea.
Hata hivyo wananchi hao waliokuwa nje ya lango kuu la mahakama waliacha kupiga kelele hizo baada ya Sabaya kuingia kwenye chumba cha mahabusu cha mahakama.
Ulinzi umeimarishwa mahakamani hapo ambapo askari magereza wenye silaha walionekana kwenye maeneo mbalimbali ya mahakama wakiwa wameficha sura zao kwa kofia na miwani.

0 Comments:
Post a Comment