Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini, (TTB), Devotha Mdachi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini, (TTB), Devotha Mdachi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha.
Waziri Dr.Ndumbaro ametoa maamuzi hayo April 10, mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo amesema uchunguzi huo hauhusiani na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
“Nafasi ya Mdachi itakaimiwa na Betrita James ambaye ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi TANAPA, hatuwezi kumchunguza Mtu akiwa kakalia kiti hichohicho” NDUMBARO
0 Comments:
Post a Comment