DUNIA YAOMBOLEZA KIFO CHA PRINCE PHILIP

 



Kufuatia kifo cha Prince Phillip, viongozi mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wametumia mtandao wa Twitter kutuma salamu za rambirambi  na miongoni mwao ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, Dkt. Tedros Ghebreyesus.

Katika ujumbe wake amesema, “nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Prince Phillip, Duke wa Edinburgh na natuma salamu za rambirambi kwa mkewe Malkia Elizabeth, familia ya kifalme na wananchi wa Uingereza.”

Naye Ngozi Okonjo-Iweala, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la biashara duniani, WTO amesema, “nimesikitishwa na kifo na natuma salamu za rambirambi kwa Malkia Elizabeth wa II, Waziri Mkuu Boris Johnson na zaidi kwa Prince William.”

David Milpass, Mkurugenzi Mkuu wa Benki  ya Dunia amemwelezea Prince Phillip kama mtu ambaye alikuwa amejitolea kwa huduma za umma na kuwa na uchanya katika maisha.

 Ametuma salamu za rambirambi kwa Malkia Elizabeth wa II, familia ya kifalme na serikali na wananchi wa Uingereza huku akisema yuko pamoja nao wakati  huu wa kipindi cha majonzi.

0 Comments:

Post a Comment