SHAHIDI AELEZA NAMNA FAMILIA YA MSHITAKIWA ILIVYOKAMATWA

 


MWENYEKITI wa Mtaa wa Korongoni, Goodluck Lekajo, (41) ameileza mahakama kuwa wazazi wa mshitakiwa Joel Kazimoto walikamatwa  na polisi mara tatu tofauti wakati wakati mshitakiwa huyo akitafutwa.


Ameeleza hayo leo mbele ya hakimu Mkazi, Pamela Meena, wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha anayesikiliza shauri hilo  wakati alipokuwa akihojiwa na wakili wa utetezi Edmund Ngemera.

Ameeleza kuwa kuna wakati mama yake Joel  alikamatwa na polisi na wakati mwingine alikamatwa binti  (hakumtaja jina) akiwa barabarani.

"Tulishakaa kikao na Sunda, (Emanuel Wado) nyumbani kwa mzee Kea (baba wa mshitakiwa) akatueleza sababu za kamata kamata watu wa familia ya Mzee Kea," ameeleza shahidi huyo wa nne upande wa jamhuri.

Lekajo ameieleza mahakama kuwa kwenye kikao walikuwa Sunda, askari polisi, Rajabu Isaya, Jeremiah ambaye ndiye alimtafutia kazi Joel nyumbani kwa Sunda na kaka yake Joel, Kazimoto.

Hata hivyo aliieleza mahakama hiyo kuwa alipata taarifa kuwa kabla ya kikao hicho Sunda na mke wake, ambaye hakumtaja jina walishafika nyumbani kwa mzee Kea mara mbili na kufanya kikao ingawa mara mara zote uongozi wa mtaa haukushirikishwa.

Lekajo ameeleza kuwa kwenye kikao kilichoitwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha ambapo hakumbuki tarehe wala mwezi, mlalamikaji akiwa familia ya mzee Kea ambao walikuwa wanalalamikia kamata kamata ya mara kwa mara ambayo walikuwa hawajui nini sababu.

Anaeleza kuwa mshitakiwa Joel alipopigiwa simu alisema kuwa kama ni kwa mkuu wa wilaya atakuja na kweli alifika.

  Awali shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa mwishoni mwa mwaka 2019 siku asiyoikumbuka alimuuzia Joel kiwanja mtaa wa Mkonoo kata ya Terati ingawa alishindwa kuwasilisha mkataba wa mauziano.

Shauri hilo limeahirishwa mpaka Mei 4, mwaka huu litakaporudi kwa upande wa jamhuri kuendelea kutoa ushahidi ambapo mshitakiwa amerudishwa mahabusu kwenye gereza la Kisongo.


0 Comments:

Post a Comment