·1959- Azaliwa Chato kaskazini magharibi mwa Tanzania
·1995- Achaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza
·2000- Ateuliwa kuwa Waziri
·2015- Achaguliwa kuwa rais kwa muhula wake wa kwanza
·2020- Achaguliwa kwa kipindi cha pili kuwa rais
·2020 Novemba tarehe 5 – Aapishwa kwa muhula wa Pili
·2021 Machi Tarehe 7- Uvumi unaanza kuenea kuhusu aliko rais Magufuli baada ya kukosa kuonekana kwa muda wa wiki moja
·2021 Machi tarehe 11 – Vyama mbali mbali vya Upinzani nchini Tanzania vyataka kujua hali ya rais Magufuli na aliko
·2021 Machi Tarehe 12 -Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akana kwamba rais Magufuli anaugua asema yupo ‘ buheri wa afya na anaendelea kuchapa kazi’
·2021 Machi Tarehe 15 – Makamu wa Rais Samia Suluhu awapa Watanzania ‘salamu’ kutoka kwa Rais Magufuli huku hofu ikizidi kuhusu hali yake na aliko
·2021 Machi, tarehe 6 - Alazwa katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme
·2021 Machi tarehe 7 - Aliruhusiwa kurejea kazini
·2021 Machi tarehe 14 - Alikimbizwa Hospitali ya Mzena Dar es Salaam kuendelea na matibabu
·2021 Machi tarehe 17 saa kumi na mbili jioni - Magufuli afariki dunia
·2021 Machi tarehe 17 Usiku – Makamu wa rais Samia Suluhu atangaza kupitia runinga kifo cha rais Magufuli .Siku 14 za maombolezo zatangazwa.Bendera kupeperushwa nusu mlingoti.
0 Comments:
Post a Comment