Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amewataka waandishi wa habari za Bunge kuepuka kutumia lugha ya kashfa,uongo na uchochezi na kutoa kauli hitimisho wakati Bunge bado linajadili suala au azimio fulani.
Aidha amewasisitiza waandishi hao kuachana na kuandika hoja/habari kishabiki bila kuzingatia upande wa pili
"Mara kadhaa waandishi wamekosea kwa kuandika mfano hoja ya Mbunge mmoja kabla ya majibu ya Waziri,Serikali au Mbunge mwingine" alisema Dkt Abbasi.
Dkt Abbasi ameyasema hayo leo wakati akitoa mada kuhusu mambo muhimu ya kuzingatiwa na waandishi wa habari za Bunge katika ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.



0 Comments:
Post a Comment