Maria na Consolata ambao ni mapacha walioungana wameaga Dunia katika hospitali ya Rufaa ya Iringa usiku wa wa Jana June 2, mwaka huu.
Maria na Consolata miezi miwili wamekuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili na siku ya tar 01/06/2018 walifikishwa katika hospitali ya Rufaa ya Iringa kwenye Chumba cha wagonjwa mahututi Yaani Intensive Care Unity ICU.
Jana usiku Maria alitangulia kuaga Dunia na dakika kumi Baadae ndipo Consolata akafuatia kufariki
Mapacha hawa walikuwa wanasomea shahada ya kwanza ya ualimu wa Sanaa katika Chuo kikuu cha Ruaha Iringa. {RUCU}.walikuwa mwaka wa kwanza wa Masomo yaani First year.
REST IN PEACE MABINTI WAZURI MARIA NA CONSOLATA
0 Comments:
Post a Comment