
"Maumbile ya Maria na Consolta ndio sababu kubwa iliyochangia kifo chao" Daktari Mseleto Nyakiloto ameeleza hayo alipozungumza na BBC.
Mseleto Nyakiloto ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji na mganga mfawidhi wa hospitali ya Iringa ameeleza chanzo kilichopelekea wasichana hao kufariki ni tatizo la njia ya hewa.
"Mmoja alitangulia na mwingine alifariki baada ya dakika kumi,Maria ndio alikuwa ana tatizo la kiafya kwa kuwa mapafu yake yalishindwa kufanya kazi na huyu mwingine alikufa kutokana na viungo vingi katika mwili wao wanavitumia kwa pamoja".Dr.Nyakiloto aeleza
(HABARI KWA HISANI YA BBC)
(HABARI KWA HISANI YA BBC)
Miguu yao ilikuwa imechukua sehemu kubwa ya mwili,
Kwa Maria mguu wake wa kulia ndio ulikuwa na nguvu wakati Consolatha ulikuwa wa kushoto na miguu yao mengine ilikuwa haifanyi kazi.
Walikuwa na vichwa viwili,mioyo miwili na mikono minne.
Na walikuwa wanatumia viongo vingine kwa pamoja kama tumbo,ini,sehemu ya uke na haja.
Maria alikuwa na matatizo ya kiafya tangu alipozaliwa ,alikuwa na shida ya kupumua ingawa licha ya kuwa alikuwa ana uwezo wa kula chakula zaidi ya mwenzie.
Maria alikuwa akila kwa niaba ya ndugu yake kwa takribani miaka mitano na nusu ndipo Consolata na yeye alipoanza kula mwenyewe.
Wanatumia baadhi ya viungo kwa pamoja
Dr Rainer Brandl aliiambia BBC Network Africa mwaka 2004, kuwa mapafu yao yalikuwa hayako sawa kwa namna ambayo hawawezi kuimili miili yao na hayawezi kuongezeka zaidi.
Na kilichobaki ni kuwaombea ili waendelee kuishi kwa matumaini.
Katika maisha yao kutegemeana ndio jambo la kubwa na kawaida katika maisha yao,kwa mfano Maria akitaka kwenda chooni atamjulisha mwenzie na vivyo hivyo kwa Consolata.
Hata hivyo daktari huyo aliongeza kwa kusema kwamba mzunguko wa hewa na damu ndio umesababisha kifo cha cha mwingine hivyo matarajio ya mmoja kupona yasingewezekana.

Aidha daktari Nyakiloto amesema mapacha wa aina hii wapo wa aina nyingi ingawa muda wa maisha yao huwa unatofautina kutokana mazingira pia; kuna wale ambao hata hawafikii hatua ya kuzaliwa,wengine wanakaa muda mfupi wanafariki na wengine ndio wanajitahidi wanafikia umri mkubwa kama ya kina Maria na Consolata wameweza kufika miaka 21.

Mwaka 2004,BBC iliandika juu ya watoto hawa mapacha ambao walikuwa na miaka sita kuwa maisha yao yako kwenye mashaka.
Tatizo kubwa ambalo lilikuwa linawasumbua ilikuwa mapafu yao yana uzito mkubwa kuliko mwili wao.
Madaktari walikuwa na hofu juu ya tatizo la mmoja linaweza kusababisha mwingine kuathirika na kuwafanyia upasuaji,kutaongeza tatizo kuwa kubwa zaidi.
0 Comments:
Post a Comment