Uongozi wa timu ya soka ya villa real inayo shiriki ligi kuu ya nchini Hispania, (LALIGA) umekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya polisi mkoani Arusha inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa.
mkurugenzi wa timu hiyo, Ammar Hayani, amesema wamefikia uamuzi huo baada ya vutiwa na amani,usalama wa Tanzania huku akisisitiza michezo ambapo amesema ili soka la Tanzania liweze kupiga hatua ni wakati muafaka wa vilabu kuongeza ushirikiano kwa vilabu vya soka kwa nchi nje ya mipaka ya tanzania.
Akizungumza viwanjani mara baada ya kupokea jezi kutoka kwa klabu hiyo ya uhispania kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi amesema vifaa hivyo vitaongeza chachu katika michezo kwa lengo la kujiweka katika nafasi nzuri katika mchezo wa soka kwa timu yao.
Klabu ya polisi Morani imemaliza nafasi ya 6 kati ya timu 15 katika mashindano ya soka ngazi ya mkoa

0 Comments:
Post a Comment