JESHI la polisi limeweka ulinzi mkali kwenye Mahakama ya Kisutu wakati
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe na viongozi wakuu wengine watano wa chama hicho wakitarajiwa kurejeshwa mahakamani hapo leo
Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard, Mashauri leo anatarajiwa kutoa uamuzi endapo viongozi hao wapatiwe dhamana wawe uraiani au waendelee kushikiliwa mahabusu kwenye gereza la Segerea mpaka kesi hiyo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Hatua ya viongozi hao kushikiliwa kwenye gereza la Segerea tokea juzi inatokana na upande wa jamhuri kuwasilisha hoja mahakamani hapo wakitaka wanyimwe dhamana kwaaslahi ya umma hoja iliyopita vikali na mawakili viongozi hao ndipo hakimu akaahirisha shauri hilo mpaka leo kwa ajili ya kusoma uamuzi.
0 Comments:
Post a Comment