MAHAKAMA YAAWAACHIA KWA DHAMANA MBOWE NA WENZAKE



Mahakama ya  Kisutu imekubali kuwapa dhamana, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watano kwa sharti kila mmoja awe na  wadhamini wawili huku kila mshtakiwa akitakiwa kusaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 20.

Pia wadhamini  watasaini kiwango hicho cha fedha ambapo  washtakiwa wakiwa nje kwa dhamana wanatakiwa kuripoti polisi mara moja kwa wiki kila siku ya alhamisi.

Uamuzi huo mdogo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri anayesikiliza shauri hilo linalovuta hisia za wengi.

Hata hivyo uamuzi huo umetolewa bila washitakiwa hao kuwepo mahakamani baada ya Ofisa wa Magereza Inspekta Shaban kuieleza mahakama  "Mbowe na wenzake wameshindwa kufika Mahakamani hapo kusomewa uamuzi wao kuhusu dhamana kwa sababu gari walilopanda limearibika."



0 Comments:

Post a Comment