#UPDATES: KAMBI RASMI YA UPINZANI KUMPELEKA LISSU NAIROBI KWA MATIBABU

Wah Wabunge. Hali ya Mhe. Lissu inaendelea kuimarika. Keshafanyiwa upasuaji wa awali.

Bunge na Serikali wako tayari kugharamia matibabu ndani ya nchi. Nimesisitiza kuwa hatuko tayari kumwacha nchi kwa sasa si kwa sababu ya uwezo wa madaktari wetu na hospitali, bali kwa sababu za kiusalama. Hawako tayari kugharamia. Tunalazimika kugharamia wenyewe.

Naendelea na mipango ya kumrusha leo kwenda Nairobi Aghakhan Hospital kupitia Dar Airport ambapo air ambulance inamsubiri.

Gharama hazijajulikana lakini ndege tu from Dom Dar Nairobi ni +_ US$10,000. Bado matibabu tutajua mbele.

Namwomba Mhe Kiwelu aanze emergecy fund mobilization. Angalao isipungue shs 500,000/- kwa Mbunge. Chama nacho kitachangia.

Nawashukuru kwa ushirikiano.

Freeman Mbowe
Mkt na KUB

Madaktari wanasema ataweza kusafirishwa baada ya saa limoja na nusu.

0 Comments:

Post a Comment