Mbunge Joseph Selasini amesema Rais wa TLS, Tundu Lissu alianza kufuatiliwa na watu waliompiga risasi mikononi, miguuni na tumboni kuanzia alipotoka bungeni.
Amesema Mbunge huyo wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alifuatiliwa na watu hao waliokuwa kwenye gari ambalo namba zake hazijafahamika mpaka nyumbani kwake kisha wakammiminia risasi.
Selasini amesema kuwa dereva wa Lissu alimweleza kuwa alibaini kuwa gari lao linafuatiliwa hivyo akamueleza Lissu.
Selasini alisema dereva alimweleza kuwa walipofika nyumbani kwa Lissu alimsihi bosi wake asishuke ndani ya gari.
"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi zisizo na idadi upande wa Lissu," alisema Selasini na kuongeza.
“Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."
Baada ya tukio hilo Lissu anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

0 Comments:
Post a Comment